Kanzu
(kwa
Kiingereza
:
tunic
) ni
vazi
la
rangi nyeupe
au nyingine ambayo tangu kale huvaliwa na
wanaume
na
wanawake
vilevile katika maeneo mengi, kama vile
bonde
la mto
Indus
na
Ulaya
, lakini siku hizi matumizi yake yamepungua. Katika
ustaarabu wa Magharibi
, sanasana imebaki katika
dini
, yaani
utawa
na
liturujia
.
Ndani ya
Afrika
kanzu huwa na
urefu
wa kufika kwenye
kifundo
cha
mguu
au kwenye
sakafu
. Hutumika kama
vazi
la kitaifa kwa
Tanzania
(ambapo hilo neno lilitumika kwa kubadilishana na kaftan) na vilevile kwa
Komoro
(ambapo huitwa/hutamkwa 'Kandu', pia kwa jina la thawb kama katika nchi za
Kiarabu
). Vazi hilo pia huvaliwa kwenye baadhi ya mikoa ya pwani ya
Kenya
. Wanaume wa
Uganda
hulichukulia kama nguo muhimu sana (Kanzu ni neno la
Kiganda
lenye asili ya
Kiswahili
ambalo humaanisha "robe" au "tunic").
Kanzu za
Uganda
zilianzishwa na
ufalme
wa
Buganda
na
wafanyabiashara
Waarabu
[1]
. Ssuuna alikuwa
Kabaka
wa kwanza wa Buganda kuvaa kanzu. Baada ya Kabaka kulipitisha hilo vazi ikawa kawaida kuvaliwa na wanaume wa Buganda wote. Kanzu ilisambaa kutoka kwa Waganda kwenda
makabila
mengine ikawa
desturi
ya taifa ya wanaume
[2]
, ingawa katika
Jamhuri
ya Uganda si vazi la kitaifa kama ilivyo kwa majirani Tanzania.
Kwa Tanzania, kanzu ilianzishwa na wafanyabiashara na
wamisionari
kutoka
Oman
ambao walifanya
dawah
. Kanzu kwa Tanzania ilikuwa ni kidhihirisho cha mavazi ya
Waarabu
. Asili ya kanzu ni kutokea
hariri
. Kwa leo, kutokana na vikwazo vya
Kiislamu
kwenye mavazi ya hariri, ikawa inatengenezwa kutumia polyester au
sintetiki
ya
vitambaa
vilivyotengenezwa kwa kufanana na hariri. Sifa za ukinzani wa kanzu za Tanzania ni pindo linaloning'inia kwenye kola
[3]
. Kwenye baadhi ya
familia
, pindo hilo huwekewa
marashi
na baadhi ya
mafuta
ya Kiafrika na Kiarabu kabla ya
sherehe
ya
harusi
. Kanzu mara nyingi huvaliwa na
kofia
maalumu.
Kwa
Kenya
, kanzu za Tanzania huvaliwa na
Waislamu
wa makabila yote.
Wakristo
huvaa kanzu (kwa kiwango kidogo) kwa matukio yasiyo rasmi, kujumlisha na
huduma
za
Kanisa
, lakini
shati
la dashiki au shati la
kitenge
hutumika kama vazi la kawaida kwenye harusi za Wakristo. Zote jamii za madhehebu huvaa kofia, kofia ndogo na kanzu. Kwa Kenya, ni desturi ya wakuu wa makabila na
maimam
wa Kiislamu kuvaa
mkia
mweusi na kanzu wanapohudhuria matukio ya kawaida. Kenya ni ya kipekee kati ya mataifa ya Afrika kwa hilo kwa kuwa ni nchi pekee isiyo na
tamaduni
za kitaifa
[4]
. Kwa kweli wanaume wa Kenya huvaa
suti
za
Ulaya
au tuxedos kwenye harusi au matukio mengine. Wengine wameanza kuvaa nguo za
Kinigeria
ambazo huitwa
Agbada
[5]
. Ndani ya Kenya,
wabunge
wanaume hutakiwa kuvaa
mitindo
ya Ulaya kwenye mikutano yao
[6]
.
Ndani ya
Afrika ya Magharibi
, vivyo hivyo kwa wingi vazi hilo lilivaliwa kwa kiasi kikubwa na watu wa Sahelia. Hapo ni pamoja na kaftan na boubou (mara nyingi huvaliwa kwenye matukio ya kawaida).
Kanzu ni vazi la asili la harusi kwa wanaume wa nchi za
Maziwa Makuu ya Afrika
. Kipindi cha kusherekea harusi bwana harusi kimila huvaa kanzu nyeupe na kofia. Ndani ya Tanzania na Kenya, bwana harusi huvaa mkia mweusi au mweupe juu ya kanzu
[3]
. Bwana harusi na wanaume wengine kwenye sherehe ya harusi huvaa kanzu na
jaketi
la suti. Ndani ya Uganda, bwana harusi huvaa jaketi la suti juu ya kanzu na vazi la mahali huwa ni gomesi.
- "Dress and Adornment."
The New Encyclopædia Britannica
. 15th edition. Volume 17. 1994.
- Payne, Blanche:
History of Costume from the Ancient Egyptians to the Twentieth Century
, Harper & Row, 1965. No ISBN for this edition; ASIN B0006BMNFS