Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kani nje
(kwa
Kiingereza
: centrifugal force)
ni
kani
inayotokea katika mfumo wa
mzunguko
na kuelekea nje. Inasababishwa na
inesha
ya
masi
ya
kitu
kilichopo katika mwendo wa mzunguko. Katika mzunguko mfululizo ni sawa na kani kitovu.
Katika
maisha
ya kila
siku
tunasikia kani nje tukitumia chombo cha
usafiri
. Tukiwa tumesimama katika
basi
linalopiga kona tunasikia jinsi gani
mwili
wetu unavyosukumwa upande wa nje. Kama
gari
linapita kona kwa
kasi
kidogo, vitu au mizigo inaweza kuanguka.
Kwa mfano:
sayari
inayozunguka
Jua
huwa na
obiti
thabiti kama kani nje ya mwendo wake ni sawa na kani ya
graviti
inayoivuta kuelekea
Jua
.
Satelaiti
inayopelekwa kwenye obiti ya
Dunia
inahitaji kurekebisha kasi yake hadi kufikia kani nje inayolingana na graviti ya Dunia.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
fizikia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kani nje
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|