Marcus Opellius Macrinus (takriban 165 ? Juni 218 ) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 11 Aprili , 217 hadi tarehe 8 Juni , 218 . Alimfuata Caracalla . Kabla Macrinus hajafa, mpwa wa Caracalla, Elagabalus alitangazwa kuwa Kaizari tarehe 18 Mei . Alimshinda Macrinus katika pigano la vita tarehe 8 Juni , na Macrinus aliuawa kisheria baadaye kidogo.