Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"
Kristo
na watakatifu Juliani na Basilisa,
Celsus na Machonila
",
mchoro
wa
Pompeo Batoni
, 1736-8.
Juliani na Basilisa
(walifariki
Antinoe
,
Misri
,
304
hivi) walikuwa
mume
na
mke
. Waliuawa kwa ajili ya
imani
ya
Kikristo
wakati wa
dhuluma
ya
kaisari
Diokletian
[1]
.
Tangu kale wanaheshimiwa kama
watakatifu
wafiadini
.
Sikukuu
yao huadhimishwa
tarehe
6 Januari
[2]
[3]
, lakini pia
7 Januari
na
9 Januari
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: