Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Johannesburg
(inayojulikana pia kama
iGoli
) ni jiji kubwa katika nchi ya
Afrika Kusini
. Ni mji mkuu wa jimbo la
Gauteng
.
Mji ulianzishwa
4 Oktoba
1886
ukakua haraka baada ya kupatikana kwa dhahabu. Siku hizi ni kitovu cha kiuchumi wa Afrika Kusini na makao ya
soko la hisa
kubwa katika
Afrika
.
Japokuwa johannesburg ni mji mkubwa lakini sio miongoni mwa miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini lakini
mahakama ya katiba
inakaa hapa.
Pia kuna jengo lililosheheni maofisi kubwa kuliko yote barani Afrika ambalo linaitwa Carlton Centre lenye ghorofa 50 kuna pia jengo refu kabisa barani afrika linaloitwa Hillbrow Tower (mita 270 au maghorofa 90).
Karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji la johannesburg huishi katika eneo la
Soweto
ambalo ni mtaa maarufu ulioengwa nje ya jiji asilia kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika wakati wa
Apartheid
(siasa ya ubaguzi wa rangi).
Jozi kama inavyojulikana na wengi ni moja kati ya miji mikubwa duniani iliyoendelea(kujengeka) sehemu ambako hakuna mto,ziwa ama bahari
ufukwe
..! Imehaririwa na
Selemani Mkonje
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Afrika Kusini
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Johannesburg
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|