Johannes Diderik van der Waals ( 23 Novemba , 1837 hadi 8 Machi , 1923 ) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi . Hasa alichunguza hali ya gesi na ya kiowevu . Mwaka wa 1910 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia .