Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jalidi
ni hali ya
baridi
ambapo
halijoto
inafikia chini ya kiwango cha
sentigredi
0. Hii ni kiwango ambako
maji
yanaanza kuganda kuwa
barafu
.
Jalidi kama halijoto inaathiri
viumbehai
na
mimea
kwa sababu huwa na
maji
katika
miili
yao. Mimea inakufa katika hali ya jalidi kama maji ndani ya
seli
zao inaganda; maji yakiganda yanapanua
mjao
wake hivyo kupasua seli. Mimea hiyo au sehemu zao zilizokufa huwa nyeusi na hali hii hutiwa jalidi pia (kwa
Kiingereza
:
black frost
).
Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa
majira ya baridi
ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika
mazingira
ya
joto
mimea hufa mara nyingi kama baridi huwa kali.
Kama hali ya jalidi inaendelea kwa
wiki
mfululizo inaathiri pia ardh,i yaani
udongo
. Ardhi yenyewe inaganda hadi
kimo
fulani kinachotegemea
muda
wa kudumu kwa jalidi. Kwa hiyo
mabomba
ya
maji
yanawekwa chini ya ardhi kwenye kimo ambako kwa kawaida jalidi haifiki. Hata hivyo, kama majirabaridi ni kali sana maji yanaweza kuganda ndani ya mabomba na kupasua bomba. Katika mazingira yenye jalidi kunatokea pia uharibifu wa
barabara
kama maji ya
mvua
yameingia katika tako la barabara au katika mapengo madogo kwenye
lami
na kuganda baadaye; maana maji yaliyoganda hupanuka kidogo na hivyo kupasua lami.
Katika mazingira baridi sana kama
Aktiki
au
Antaktiki
jalidi inaingia katika udongo hadi kimo cha
mita
kadhaa. Katika mazingira hayo
majirajoto
ni mafupi mno, hivyo kuna sehemu za juu za ardhi pekee zinazopoa lakini chini yake bado kuna
jalidi ya kudumu
(ing.
permafrost
). Hii inazuia
uoto
wa
miti
na kutokea kwa
tundra
kwa mfano katika maeneo mapana ya
Urusi
wa
Kaskazini
na
Alaska
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Jalidi
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|