Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ekolojia
(
gir.
ο?κο?
oikos
"nyumba" + -λογ?α
logia
"elimu ya..") ni tawi la
biolojia
inayoangalia
viumbehai
na mazingira yao, kama ni hali asilia au viumbehai wengine.
Kwa hiyo ukiuliza jinsi gani
samaki
wanahusiana na samaki na
wanyama
wengine na
binadamu
pamoja na
mimea
na hali ya
maji
wanamoishi unauliza maswali kuhusu ekolojia yao.
Wataalamu
wa ekolojia huchungulia kila kitu kuanzia
bakteria
ndogo katika
myeyusho
wa kuwalisha hadi athira ya
msitu wa mvua
kwa
halihewa
ya
dunia
.
Ekolojia inalenga kuelewa jinsi gani pande mbalimbali za
uhai
duniani zinahusiana na mazingira yao. Kila
spishi
ya viumbehai inategemea
makazi
maalumu kwa kudumisha
maisha
yake. Hapo ekolojia inachungulia pia athira ya mabadiliko yanayosababishwa na binadamu kwa makazi haya na ekolojia yao.
Kwa mfano matumizi ya
madawa
ya kuua
wadudu
katika
kilimo
yanaweza kubadilisha ekolojia ya makazi kwa
nyuki
; kupotea kwa nyuki katika eneo kunaathiri pia kustawi wa mimea inayotegemea nyuki kwa kuzalisha
matunda
yao.
Kwa hiyo ekolojia ni elimu ya msingi kwa kutambua
uharibifu wa mazingira
na kutambua hatua muhimu ya
kuhifadhi mazingira
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
biolojia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ekolojia
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|