Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ijumaa Kuu
ni
siku
ya
Ijumaa
kabla ya
Pasaka
ambapo
Wakristo
wengi
duniani
wanaadhimisha
kifo
cha
Yesu Kristo
msalabani
.
Kufuatana na taarifa za
Injili
nne
katika
Biblia ya Kikristo
,
Yesu
alisulubiwa
siku kabla ya
Sabato
(au
Jumamosi
), yaani Ijumaa. Mahali pa kumsulubisha palikuwa
kilima
cha
Golgotha
kilichokuwepo wakati ule nje ya
kuta
za
mji
wa
Yerusalemu
.
Kadiri ya
Injili
ya
Mtume Yohane
, kesho yake ilikuwa
Sabato
na pia
Pasaka
, jambo lisilotokea kila mwaka. Kwa sababu hiyo
wataalamu
mbalimbali wameweza kukadiria ilikuwa
tarehe
7 Aprili
30
.
Sikukuu
hii haina tarehe thabiti katika
kalenda
ya kawaida. Ilhali hutangulia Pasaka inafuata pia mabadiliko ya tarehe za Pasaka. Pamoja na
mapokeo
yaliyo tofauti kati ya
Ukristo wa Magharibi
(
Wakatoliki
na
Waprotestanti
wengi) na
Ukristo wa Mashariki
(
makanisa ya Kiorthodoksi
na
Wakatoliki wa Mashariki
), kuna tarehe
mbili
tofauti za Pasaka, na hivyo pia kila mwaka kuna tarehe mbili tofauti za Ijumaa Kuu.
Mwaka
|
Ukristo wa
Magharibi
|
Ukristo wa
Mashariki
|
2018
|
30 Machi
|
06 Aprili
|
2019
|
19 Aprili
|
26 Aprili
|
2020
|
10 Aprili
|
17 Aprili
|
2021
|
02 Aprili
|
30 Aprili
|
2022
|
15 Aprili
|
22 Aprili
|
Ijumaa kuu ni sehemu ya
Juma Kuu
linaloanza kwa adhimisho la
Yesu
kuingia mji huo akishangiliwa kama
mfalme wa Wayahudi
(yaani
Masiya
au
Kristo
). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa
wiki
, yaani
Jumapili ya matawi
.
Ijumaa kuu ni pia sehemu ya
siku tatu kuu za Pasaka
zinazoadhimisha mateso na
kifo chake
(
Ijumaa
), kulala
kaburini
(
Jumamosi
), na hatimaye
kufufuka
kwa
utukufu
(
Jumapili
), kwa ufupi:
- Yesu mteswa,
- mzikwa na
- mfufuka.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ijumaa Kuu
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|