Kitabu cha Hosea
ni kimojawapo kati ya
vitabu
vya
Tanakh
(yaani
Biblia ya Kiebrania
), na hivyo pia vya
Agano la Kale
katika
Biblia ya Kikristo
.
Kwa kuwa kina
sura
14 tu, kimepangwa tangu zamani za kale kati ya vitabu 12 vya
Manabii Wadogo
.
Hata hivyo umuhimu wake katika maendeleo ya
Ufunuo
wa Mungu kwa
Israeli
ni mkubwa, kwa jinsi kilivyoathiri vitabu vilivyofuata hadi
Kitabu cha Ufunuo
.
Kama vitabu vingine vyote vya
Biblia
, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa
historia ya wokovu
ili kukielewa kadiri ya maendeleo hayo.
Nabii
Hosea
alitokea
Ufalme wa Israeli
(
Kaskazini
) ambapo alifanya
kazi
ya
unabii
kuanzia miaka ya mwisho ya
utawala
wa
Yeroboamu II
(
786
-
746 KK
) hadi karibu na maangamizi ya mwaka
722 KK
ambayo aliyatabiri kutokana na
uasi
wa kidini wa Waisraeli wenzake.
Wakati huohuo walifanya kazi pia
Amosi
upande wa Kaskazini, halafu
Isaya
katika
Ufalme wa Kusini (Yuda)
.
Hosea alitangaza hasa
upendo
wa
Mungu
kwa
taifa
lake.
Adhabu
zenyewe zilizotabiriwa zinaelezwa kuwa zimetokana na upendo huo wenye
wivu
ambao unalenga kuwarudisha Waisraeli katika upendo mwaminifu wa
kiuchumba
.
Hosea alikuwa wa kwanza kumfananisha
Mwenyezi Mungu
na
mume
mwaminifu wa
mwanamke
malaya
.
Maisha
ya nabii mwenyewe yalikuwa na
tabu
ya namna hiyo ili yawe kwa wote kielelezo che uhusiano kati ya Mungu na watu wake.
Alidai
Waisraeli
wawe waaminifu kwa Mungu pekee, pamoja na kusisitiza kuwa
dini
haiwezi kuishia katika
ibada
zisizohuishwa na upendo, la sivyo wataangamia.
Mwanzoni mwa kitabu, Hosea aliagizwa na Mungu
amuoe
kahaba
atakayemzalia
wanaharamu
anayewakilisha taifa la
Israeli
lililoabudu
miungu
mingine pia kama
asili
ya
ustawi
wake na kutegemea
mbinu
za kisiasa ili kujidumisha salama.
Kwa kuwa hawakumtegemea Mungu wao, Hosea aliwatabiria Waisraeli watapelekwa
uhamishoni
huko
Ashuru
.
Kama vile mke wa Hosea alivyoweza kujirekebisha, hivyo hata Israeli ikitubu itaokoka na kufaidika na
baraka
za Mungu.
|
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kitabu cha Hosea
kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|