Historia ya awali
(kwa
Kiingereza
:
prehistory
) ni kipindi kirefu sana cha
historia
, kikichukua miaka yote tangu
binadamu
walipotokea
duniani
mpaka
historia andishi
ilipoanza (huko
Mesopotamia
miaka 3,300 hivi
KK
).
[1]
Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.
Katika
lugha
nyingi
msamiati
ni
kabla ya historia
(k.mf. kwa
Kiingereza
ni pre-history), ambao unatokana na maneno ya
Kigiriki
προ, pro, yaani "kabla" na ιστορ?α, istoria, yaani "historia").
Paul Tournal
mwanzoni alitunga neno la
Kifaransa
“Pre-historique” katika kuelezea
ugunduzi
aliofanya katika
mapango
ya
kusini
mwa
Ufaransa
.
Neno hilo lilitumika katika Ufaransa kuanzia
miaka ya 1830
kuelezea kipindi kabla ya
uandishi
, na baadaye likaingizwa na
Daniel Wilson
katika
Kiingereza
mwaka
1851
.
Sehemu kubwa kabisa ya historia ya binadamu ilitokea kabla ya maandishi kugunduliwa. Kuhusu zamani hizo tunapata
habari
kutokana na
utafiti
wa
akiolojia
.
Kwa njia hiyo tunakuta mabaki ya ya siku zile kama vile
vifaa
,
majengo
au pia uchoraji kwenye kuta za mapango lakini tunakosa maelezo jinsi yanavyopatikana tangu watu waanze kuandika kumbukumbu.
Kati ya vipindi vya historia ya awali ni
zama za mawe
. Wakati huo wote watu walipiga hatua muhimu ya maendeleo, kama vile
kubuni
vifaa vya kwanza,
kilimo
, na kujenga
vijiji
na
miji
ya kwanza.
Hata vyanzo vya
teknolojia
za
metali
, kama
zama za shaba
na
zama za chuma
, vilitokea kabla ya kugundua maandishi katika sehemu nyingi za dunia.
Lakini mifano ya kwanza ya
utamaduni
wa kimaandishi ilitokea wakati wa kubuni matumizi ya
shaba
na
bronzi
huko
Misri
na
Mesopotamia
.
- ↑
Shotwell, James Thomson. An Introduction to the History of History. Records of civilization, sources and studies. New York: Columbia University Press, 1922.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Historia ya awali
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|