Henri Dunant ( 8 Mei 1828 - 30 Oktoba 1910 ) alikuwa mwandishi na mfadhili wa nchi ya Uswisi . Mwaka wa 1859 alianzisha Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu . Pia alisababisha Mapatano ya Geneva . Mwaka wa 1901 , pamoja na Frederic Passy , alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani .