Hendrik Antoon Lorentz ( 18 Julai 1853 ? 4 Februari 1928 ) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi . Alitafiti nadharia ya elektroni . Pia alichunguza nadharia ya Albert Einstein ( Relativity Theory ) na ya kwanta . Mwaka wa 1902 , pamoja na Pieter Zeeman alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia .