Heinrich Otto Wieland ( 4 Juni 1877 ? 5 Agosti 1957 ) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani . Alihariri kumbukumbu za kikemia za Justus von Liebig . Pia alichunguza mifumo ya kikemia ya sumu za uyoga na asidi ya nyongo. Mwaka wa 1927 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia .