Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gurudumu
ni mtambo mwenye umbo la
duara
. Linaruhusu gari kutembea; magurudumu yanazunguka na mzigo (mfano gari) juu yake unaenda mbele kwa kutumia nguvu kidogo.
Gurudumu linapunguza
msuguano
; badala ya msunguano wa kitu chote kinachosogea mbele kwenye ardhi kuna msuguano wa sehemu ndogo ya gurudumu na msuguano wa gurudumu kwenye
ekseli
yake. Msuguano kati ya ekseli na gurudumu unapunguzwa kwa njia ya kutia mafuta au kuweka
beringi gololi
kati ya gurudumu na ekseli.
Sehemu kubwa ya usafiri kwenye nchi kavu hutegemea magurudumu kwa mfano
motokaa
, lori,
reli
ya kawaida na
baisikeli
. Magurudumu ni pia sehemu kubwa ya machine nyingi.
Tangu karne ya 19 magurudumu yanaviringishwa kwa
matairi
ya mpira na hii inanyosha mwendo wake.
Wataalamu wa historia huamini ya kwamba watu wa
Babeli
walikuwa wa kwanza kugundua gurudumu na kulitumia tangu mwaka
4000 KK
. Watu wa
China ya Kale
waliligundua pia mnamo 2800 KK.
Ustaarabu za
Amerika ya Kale
kama
Inka
na
Azteki
waligundua gurudumu pia likatumiwa kwa vitu vya kucheza watoto lakini halikuwa na matumizi ya kikazi.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
fizikia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Gurudumu
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|