Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Greenland
(kwa
Kiswahili
Grinilandi
pia; kwa
Kikalaallisut
:
Kalaallit Nunaat
= Nchi ya Wagreenland) ni nchi ya kujitawala chini ya
ufalme
wa
Denmark
lakini haihesabiwi kuwa sehemu ya Denmark yenyewe.
Eneo la Greenland ni kubwa, lakini idadi ya wakazi ni ndogo sana kwa sababu sehemu kubwa ya nchi (75%) imefunikwa na
ganda
nene la
barafu
.
Jina
la
Kiswahili
limetokana na lile la
Kiingereza
"Greenland", ambalo ni
tafsiri
ya jina la
Kidenmark
"Grønland", linalomaanisha "nchi yenye
rangi
ya ma
jani
mabichi".
Jina hilo Greenland lilitungwa miaka 1000 iliyopita, kwa sababu wakati ule
hali ya hewa
duniani
ilikuwa na
joto
zaidi, na hapakuwa na barafu nyingi kama leo.
Ki
jiografia
Greenland,
kisiwa
kikubwa kuliko vyote
duniani
, ni sehemu ya
bamba la Amerika ya Kaskazini
lakini ki
historia
na ki
siasa
kwa
karne
kadhaa imekuwa na
uhusiano
wa karibu na
Skandinavia
(
Ulaya ya Kaskazini
).
Mlima
wa juu wa Greenland ni
Mlima Gunnbjørn
(m 3,694 juu ya
UB
) katika
Watkins Range
.
Barafuto
ya
Sermeq Kujatdlek
upande wa
magharibi
wa Greenland.
Mji mkuu
ni
Godthaab
inayoitwa
Nuuk
(17,000).
Wananchi wengi (89.5%) ni wakazi asilia wenye asili ya
Asia
, ingawa wengi wao wana pia
damu
ya
Kizungu
kwa asilimia 25.
Lugha
yao ndiyo
lugha rasmi
pekee tangu mwaka
2009
. 8.6% ni
Wazungu
wenye asili ya Skandinavia na wanaongea
Kidenmark
ambacho kinaendelea kutumiwa na wote katika nafasi kadhaa. Wakazi wengi wanaweza kuongea lugha zote mbili.
Upande wa
dini
, walio wengi ni
Wakristo
(96.1%), hasa
Walutheri
(85%).
Greenland inaongoza duniani kwa
asilimia
ya watu
wanaojiua
, pamoja na kuwa na idadi kubwa ya
walevi
.
Grønland
- Bardarson, I. (ed. Jonsson, F.) "Det gamle Grønlands beskrivelse af Ivar Barðarson (Ivar Bardsson)", (Copenhagen, 1930).
- CIA World Factbook
, 2000.
- Conkling, P. W.
et al.
2011. The Fate of Greenland: Lessons from Abrupt Climate Change, co-authored with Richard Alley, Wallace Broecker and George Denton, with photographs by Gary Comer, MIT Press, Cambridge, MA.
- Lund, S. 1959. The Marine Algae of East Greenland. 1. Taxonomical Part.
Meddr Gronland.
156(1), pp. 1?245.
- Lund, S. 1959. The Marine Algae of East Greenland. 11. Geographic Distribution.
Meddr Gronland.
156, pp. 1?70.
- Steffen, Konrad
, N. Cullen, and R. Huff (2005). "Climate variability and trends along the western slope of the Greenland Ice Sheet during 1991?2004,"
Proceedings of the 85th American Meteorological Society Annual Meeting
(San Diego).
- Sowa, F. 2013.
Indigenous Peoples and the Institutionalization of the Convention on Biological Diversity in Greenland.
In:
Arctic Anthropology.
50(1), pp. 72-88.
- Sowa, F. 2013.
Relations of Power & Domination in a World Polity: The Politics of Indigeneity & National Identity in Greenland.
In: Heininen, L.
Arctic Yearbook 2013. The Arctic of regions vs. the globalized Arctic.
Akureyri: Northern Research Forum, pp. 184-198.
www.arcticyearbook.com/ay2013
Archived
19 Februari 2015 at the
Wayback Machine
.
- Sowa, F. 2014.
Greenland.
in: Hund, A.
Antarctica and the Arctic Circle: A Geographic Encyclopedia of the Earth’s Polar Regions.
Santa Barbara, CA: ABC-CLIO, pp. 312-316.
WikiMedia Commons
- Taarifa za jumla
- Serikali
- Ramani
- Vyombo vya habari
- Biashara
- Safari
- Mengineyo
|
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
|