Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ghuba ya Hudson
(
ing.
:
Hudson Bay
,
far.
: baie d'Hudson,
Kiinuktitut
: Kangiqsualuk ilua) ni ghuba kubwa ya
Bahari Atlantiki
(
Bahari ya Labrador
) ndani ya ardhi ya
Kanada
mashariki. Eneo lake ni 819,000 km² (ni kubwa kuliko nchi ya
Zambia
). Ina umbo kama ziwa la ndani ya nchi kavu ikiunganishwa na bahari ya Labrador kwa njia nyembamba ya
mlango wa Hudson
yenye upana wa kilomita 64. Kuna mlango mdogo wa pili huu ni
mlango wa Fury na Hecla
.
Pwani zakle zinapaka na majimbo ya
Nunavut
,
Manitoba
,
Ontario
na
Quebec
.
Ghuba imepokea jina lake kutokana na mpelelezi Mwingereza
Henry Hudson
aliyekuwa mzungu wa kwanza kufika hapa mwaka 1610 kwa meli yake
Discovery
.
Britannica Online-Hudson Bay