Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gda?sk
(kwa
Kijerumani
:
Danzig
) ni
mji
wa
bandari
kaskazini mwa
Poland
kule ambako
mto
Vistula
unaishia katika
Bahari Baltiki
.
Mji una wakazi wapatao 500,000 na bandari muhimu zaidi ya Poland.
[1]
Mji ukikuwepo tayari mnamo
mwaka
900
BK
na tangu mwaka
979
eneo lake liliingizwa mara ya kwanza katika
milki ya Poland
.
Katika
karne ya 13
mtemi
Swantopolk
alikaribisha
walowezi
Wajerumani
kuanzisha mji chini ya utaratibu wa kwao nyumbani. Mji huu wa Kijerumani ulikua na kuwa mji muhimu wa
biashara
na tasnifu ikaungana na makazi ya awali ya wazalendo.
Mji wa Danzig (
jina
la Kijerumani) uliendelea kuwa mji wa
utamaduni
wa Kijerumani lakini kwa
karne
kadhaa ulikuwa
mji wa kujitawala
chini ya
Dola la Wamisalaba
Wajerumani na baadaye chini ya
mfalme
wa Poland.
Baada ya magawio ya Poland ulikuwa mji wa
Prussia
tangu
1796
na baadaye mji wa Ujerumani.
Baada ya
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
Danzig ilitengwa na
Ujerumani
na kuwa
Dola-mji
hadi kuvamiwa na Ujerumani mwaka
1939
. Mwisho wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
mwaka
1945
/
1946
wakazi Wajerumani walifukuzwa na mji wote pamoja na maeneo ya
mashariki
mwa Ujerumani vilipata kuwa sehemu ya Jamhuri ya Poland. Sasa jina lake ni Gdansk.
Mji ulioharibika sana
vitani
ukajengwa upya kwa kuiga
majengo
ya awali. Katika miaka ya
utawala
wa
kikomunisti
katika Poland Gdansk iliendelea kuwa
kitovu
cha upinzani na mahali ambako chama cha
Solidarnosc
kilianzishwa.
- ↑
"About Port"
.
Port of Gdansk Authority
. Iliwekwa mnamo
2009-11-05
.