Encyclopædia Britannica
ni
kamusi elezo
kubwa na moja kati ya kamusi elezo iliyo-maarufu zaidi. Inaandikwa kwa lugha ya
Kiingereza
. Kamusi elezo hii huchapishwa na kampuni binafsi ya
Encyclopaedia Britannica, Inc
. Awali ilikuwa ikichapishwa kwenye karatasi tu, lakini hivi karibuni imepanuka na kuwa na
dijiti
, au matoleo ya kompyuta vilevile. Kamusi elezo hii imegawanyika katika vitabu vingi sana. Makala za kwenye vitabu zimepangwa kwa mtindo wa kialfabeti. Kumekuwa na matoleo yake ambayo ni kwa ajili ya watoto vilevile. Hii ni kamusi elezo kubwa sana ya kuchapishwa. Kamusi elezo iliyo-kubwa ziadi ni
Wikipedia
. Watu wengi huhesabia kwamba ni kamusi elezo bora, kwa sababu ipo sahihi na ina mambo mengi.
Kamusi elezo hii awali ilikuwa ndogo sana, toleo la kwanza lilikuwa na vitabu vitatu na ilitolewa mnamo mwaka wa 1768. Polepole likawa kubwa zaidi. Toleo jipya, toleo la 15, sasa lina vitabu takriban 29, jumlisha vitabu viwili ambavyo ni faharasa. Pia imemjulisha kitabu cha ziada kiitwacho
Propaedia
, kwa ajili ya kuainisha
ufahamu
. Vitabu 29 vimeumba
Macropaedia
na
Micropaedia
. Macropædia ni kikubwa kuliko vingine, chenye makala yenye maelezo zaidi ambazo pia zaweza kuwa na kurasa 300, -metengenezwa kwa vitabu 17, wakati Micropædia ni kidogo ambacho kawaida huwa na makala fupi na maneno machache chini ya 750. Micropædia hutumika kwa ajili ya kutazama kwa haraka zaidi, lakini iwapo utahitaji habari zaidi basi inakubidi utumie Macropædia. Kila kitabu kimoja ni kikubwa sana, zaidi ya kurasa 1,000 kwa kitabu. Kuna vitabu vya mwaka. Kila mwaka, kitabu kimechapishwa kuhusu matukio ya mwaka huo.
Makala za kwenye Britannica ni kwa ajili ya watu wazima walio-elimika, si kwa ajili ya watoto, na imeandikwa na wahariri takriban 100 na wachangiaji wataalamu zaidi ya 4,000. Watu wengi hudhania ni kamusi elezo bora, lakini
Wikipedia
bado inabaki kuwa maarufu kwa kuwa matumizi yake ni bure. Britannica ni kamusi elezo ya kale kwa lugha ya Kiingereza mpaka sasa. Ilianza kuchapishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka kati ya 1768 na 1771 huko mjini
Edinburgh
,
Uskoti
na kukua kwa umaarufu mkubwa, ikiwa na toleo lake la tatu mnamo
1801
ikiwa imeongeza vitabu 21.
Ukubwa wa vitabu vya Britannica karibia vyote vinafanana kwa takriban miaka 70, ikiwa na maneno yapatayo milioni 40 ikiwa ni nusu ya mada zilizopo ndani ya vitabu vyenyewe. Kamusi elezo hii awali ilikuwa ikimilikiwa na
Uingereza
. Kwa sasa inamilikiwa na
Marekani
, lakini bado inaandikwa kwa
Kiingereza cha Uingereza
. Muda wa ziada, kamusi elezo hii imekuwa na kipindi kigumu cha upatikanaji wa fedha, kitu ambacho kamusi elezo nyingi huzikumba.
Britannica imekuwa ikimilikiwa na watu tofauti, ikiwa ni pamoja na wachapishaji wa Kiskoti
A & C Black
,
Horace Everett Hooper
,
Sears Roebuck
na
William Benton
. Encyclopædia Britannica, Inc. inamilikiwa na
Jacqui Safra
, bilionea mwigizaji wa
Uswisi
. Teknolojia ya habari imekuwa vyema zaidi hivi karibuni na imekuwa kamusi elezo ya kielektronikia zaidi kama vile
Microsoft
Encarta
na
Wikipedia
zimefanya watu kuto nunua kamusi elezo za kuchapishwa tena.
[1]
Hata hivyo bado inaweza kusalia, Encyclopædia Britannica, Inc. inaendelea kuwaambia watu kwamba
Britannica
ni nzuri na ipo sahihi zaidi, wametengeneza kamusi elezo ya bei rahisi, na kutengeneza matoleo ya kielektroni kwenye
CD-ROM
,
DVD
na
Tovuti
.
Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1930, kampuni pia imekuwa ikitafutia masoko ya kazi za faida ya haraka.
[2]
Matoleo ya Encyclopedia Britannica
Toleo
|
Mwaka
|
Idadi ya vitabu ya toleo
|
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
11.
12.
13.
14.
15.
16
|
1768-1771
1777-1784
1788-1797, 1801 sup.
1801-1809
1815
1820-1823, 1815-1824 sup.
1830-1842
1852-1860
1870-1890
1902-1903
1910-1911
1921-1922
1926
1929-1973
1974-1984
tangu 1996-2004
|
3
10
18 + 2 nyong.
20
20
20 + 2 nyong.
21
21 + index
24 + index
toleo la 9 + 9 nyong.
29
toleo la 11 + 3 nyong.
toleo la 11 + 6 nyong.
24
28
32
|
Toleo la 16 la 2004 lina makala 75,000 yenye maneno milioni 44. Vitabu vyake 32 zaweza kunununuliwa kwa
USD
1,400 kwa umbo la karatasi. Zapatikana pia kwa bei nafuu kama CD au DVD na kusomewa kwa compyuta.
|
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Encyclopedia Britannica
kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|