Emil Theodor Kocher ( 25 Agosti 1841 ? 27 Julai 1917 ) alikuwa daktari mpasuaji kutoka nchi ya Uswisi . Alifanya na kuboresha pasuaji nyingi, hasa ya tezi dundumio . Mwaka wa 1909 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba .