Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuhusu malkia mwingine mwenye jina hili ona
Elizabeth I wa Uingereza
Elizabeth II
alikuwa
malkia
wa
Ufalme wa Muungano
wa
Britania
(
Uingereza
na
Welisi
na
Uskoti
) na
Ireland Kaskazini
tangu
mwaka
1952
hadi kufariki
dunia
tarehe
8 Septemba
2022
. Alikuwa malkia kwa miaka 70 na siku 214. Katika
historia
yote ya
dunia
wako
watawala
wachache waliodumu
madarakani
muda
mrefu kuliko yeye
[1]
[2]
. Soma zaidi
wasifu wake hapa
Anafuatwa na
mwana
wake wa kwanza,
Charles III wa Uingereza
.
Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini
London
tarehe
21 Aprili
1926
kama
mtoto
wa kwanza wa mfalme
George VI wa Uingereza
na Elizabeth Bowes-Lyon.
Alitangazwa kuwa malkia tarehe
6 Februari
1952
mara moja baada ya
kifo
cha
baba
yake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea
Kenya
iliyokuwa bado
koloni
la Uingereza akatembelea
milima
ya
Aberdare
.
Alipokea
taji
katika
ibada
rasmi tarehe
2 Juni
1953
kwenye
kanisa
la
Westminster Abbey
.
Kama mkuu wa
Jumuiya ya Madola
alikuwa pia
mkuu wa dola
wa nchi zifuatazo ndani ya jumuiya hii
[3]
:
Katika nchi zote aliposhika
cheo
hakuwa na
mamlaka
ya kiserikali ila alitawala kama
mfalme wa kikatiba
katika muundo wa
serikali ya kibunge
.
Marejeo
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Elizabeth II wa Uingereza
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|