Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Einigkeit und Recht und Freiheit
("Umoja na haki na uhuru") ni maneno ya kwanza ya wimbo wa taifa la
Ujerumani
. Wimbo huo ulitungwa kiasili na mshairi
Hoffmann von Fallersleben
mwaka 1841 kama "wimbo la Wajerumani" (
Lied der Deutschen
) likiwa na mabeti matatu. Lakini beti ya tatu pekee inayokubaliwa kama wimbo la taifa. Muziki yake iliandikwa na
Joseph Haydn
.
Beti asilia ya kwanza inajulikana kutokana na chanzo chake "Ujerumani juu ya yote" (
Deutschland, Deutschland uber alles
) lakini baada ya maarifa ya utaifa mkali katika karne ya 20 uliopeleka nchi katika vita kuu mbili Wajerumani wengi hawapendi tena beti hii hivyo haitumiki tena.
Maeneo yaliyokaliwa na Wajerumani wakati wa karne ya 19
Joseph Haydn alitunga muziki hii kwa heshima ya
Kaisari
Franz
wa
Austria
na
Dola Takatifu la Kiroma
likawa wimbo la taifa la Austria hadi mwisho wa ufalme mwaka 1918.
Muziki latumiwa pia kwa nyimbo za kanisani katika nchi mbalimbali.
Mshairi August Heinrich Hoffman von Fallersleben alitunga shairi kwa ajili ya muziki hii mwaka
1841
. Wakati huu Ujerumani iligawanyika katika madola mengi madogo. Kati ya wananchi hamu ilikuwa kubwa kuungana lakini wanasiasa katika kila sehemu hawakuona faida kuachana na hali halisi. Kwa wibo wake alitaja mipaka ya ameneo walipokaa watu waliosema Kijerumani katika madola mbalimbali, wengi ndani ya mipaka ya Shirikisho la Ujerumani lakini pia wengine nje yake. Alitaka kutamka tumaini alke wote wataunganishwa siku moja.
Baada ya vita mbili maeneo makubwa yaliyokaliwa na wasemaji wa Kijerumani wakati wa Hoffmann yako chini ya nchi nyingine na wakazi wa awali hawako tena; ama walizoea lugha nyingine au walifukuzwa hasa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kwa sababu hii majirani wa Ujerumani waliona maneno ya bei ya kwanza kwa mashaka, na Wajerumani wenyewe hawakutaka tena kuimba majina ya mito ambayao sasa ni sehemu ya mataifa mengine kwa hiyo hawatumii beti ya kwanza tena.
Katika karne ya 19 wimbo la Hoffmann lilipendwa na watu lakini halikuwa wimbo la kitaifa lililokuwa wimbo la kumsifu kaisari hadi 1918. 1922 lilitangazwa kuwa wimbo la taifa katika jamhuri ya Ujerumani; baada ya vita kuu ya pili rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
alitangaza beti ya tatu kama wimbo la taifa lakini katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani
walikuwa na nyimbo tofauti.
Tangu 1990 beti la tatu ni wimbo la Ujerumani iliyounanika.
|
|
|
- D
eutschland, Deutschland uber alles,
- uber alles in der Welt,
- wenn es stets zu Schutz und Trutze
- bruderlich zusammenhalt.
- Von der Maas bis an die Memel,
- von der Etsch bis an den Belt,
- |: Deutschland, Deutschland uber alles,
- uber alles in der Welt! :|
|
- U
jerumani, Ujerumani juu ya yote
- juu ya yote duniani
- kama muda wote kwa ulinzi
- inasimama kindugu
- kutoka mto
Meuse
(upande wa magharibi)
hadi mto
Neman
(upande wa mashariki)
,
- kutoka mto
Adige
(upande wa kusini mpakani wa Italia)
hadi
Belt
(Bahari upande wa kaskazini /
Denmark
)
.
- |: Ujerumani, Ujerumani juu ya yote
- juu ya yote duniani. :|
|
|
- D
eutsche Frauen, deutsche Treue,
- deutscher Wein und deutscher Sang
- sollen in der Welt behalten
- ihren alten schonen Klang,
- uns zu edler Tat begeistern
- unser ganzes Leben lang. -
- |: Deutsche Frauen, deutsche Treue,
- deutscher Wein und deutscher Sang! :|
|
- W
anawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,
- divai ya Kijerumani na nyimbo za Kijerumani
- ziendelee kuwa kote duniani
- na sifa zao njema
- na kutuhamasisha kutenda mema
- kwa muda wa maisha yetu yote.
- |: Wanawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,
- Wanawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,
|
Beti ya tatu - Wimbo rasmi la Taifa la Ujerumani
[
hariri
|
hariri chanzo
]
|
- E
inigkeit und Recht und Freiheit
- fur das deutsche Vaterland!
- Danach lasst uns alle streben
- bruderlich mit Herz und Hand!
- Einigkeit und Recht und Freiheit
- sind des Gluckes Unterpfand;
- |: bluh im Glanze dieses Gluckes,
- bluhe, deutsches Vaterland. :|
|
- Umoja na haki na uhuru
- kwa nchi ya Kijerumani
- Huku tushikamane sisi sote
- kindugu kwa moyo na mkono
- Umoja na haki na uhuru
- ni hakikisho la raha
- |: Ustawi katika mwangaza wa raha hiyo,
- Ustawi nchi yetu ya Kijerumani :|
|