Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa
Dubu Mkubwa
Dubu Mkubwa
(kwa
Kilatini
na
Kiingereza
Ursa Major
)
[1]
ni
jina
la
kundinyota
kubwa kwenye
angakaskazi
ya
Dunia
yetu.
Jina
Ursa Major (Dubu Mkubwa) ni kati ya makundinyota yaliyootambuliwa tangu zama za kale katika mataifa mengi. Mabaharia Waswahili waliijua kama Dubu Mkubwa.
[2]
wakitafsiri jina la
Kiarabu
???? ??????
ad-dubb al-?akbar
. Waarabu waliwahi kutafsiri jina la
Wagiriki wa Kale
waliosema Μεγ?λη ?ρκτο?
megale arktos
. Mataifa mbalimbali waliiona kama dubu; Mgiriki
Aristoteli
alieleza jina hili kutokana na mahali pake katika kaskazini na imani kuwa dubu ni mnyama mkubwa wa pekee anayeweza kuishi katika mazingira ya baridi kali.
Mataifa wanaotumia
lugha za Kigermanik
waliona hapa gari kubwa wakitazama nyota saba angavu zaidi;
α
,
β
,
γ
na
δ
kama matairi ya gari na
ε
,
η
na
ζ
kama mpini wa gari. Katika
Uingereza
na
Marekani
nyota hizi 7 zinajulikana pia kwa jina la "Big Dipper" zikitazamiwa kama upawa mkubwa wa kuchotea maji.
Ursa Major ilikuwa moja ya makundinyota 48 yaliyo orodheshwa na
Klaudio Ptolemaio
. Hii ilithibitishwa na
Umoja wa Kimataifa wa Astronomia
katika orodha ya makundinyota 88 za kisasa iliyotolewa mwaka 1930. Kifupi rasmi ni ‘Uma’
[3]
[4]
Mahali pake
Dubu Mkubwa - Ursa Major iko karibu na
ncha ya anga
ya kaskazini. Kwa hiyo inafika tu kidogo juu ya upeo wa macho kwa mtazamaji wa
Tanzania
; picha inaonyesha anga jinsi inavyoweza kutazamiwa huko
Lamu
-
Kenya
.
Inapakana na makundinyota jirani ya
Tinini
(
Draco
)
,
Twiga
(
Camelopardalis
)
,
Pakamwitu
(
Lynx
)
,
Simba Mdogo
(
Leo Minor
)
,
Asadi
(
Leo
)
,
Nywele za Berenike
(
Coma Berenikes
)
,
Mbwa Wavindaji
(
Canes Venatici
)
na
Bakari
(
Bootes
)
.
Nyota
Dubu Mkubwa - Ursa Major ni kundinyota kubwa lenye nyota nyingi.
Nyota angavu zaidi ni ε Epsilon Ursae Majoris inayojulikana pia kama
Alioth
yenye
mwangaza unaoonekana
wa
mag
1.76 ikiwa umbali wa
miakanuru
81 kutoka Duniani.
[5]
Nyota angavu ya pili ni
Dubhe
au α Alpha Ursae Majoris
[6]
.
ζ Dzeta Ursae Majoris au Mizar ni nyota ya katikati kwenye "mpini" wa sehemu inayoitwa gari au Dipper. Ni
nyotamaradufu
inayotambuliwa kwa macho matupu.
Jina la
(
Bayer
)
|
Namba ya
Flamsteed
|
Jina
(
Ukia
)
|
Mwangaza
unaoonekana
|
Umbali
(
miakanuru
)
|
Aina ya spektra
|
ε
|
77
|
en:Alioth
|
1,69 bis 1,83
|
81
|
A0p
|
α
|
50
|
Dubhe
(
Dhahari ya Dubu
)
|
1,81
|
124
|
K1II-III
|
η
|
85
|
Alkaid (
Kaidi
)
|
1,86
|
101
|
B3 V
|
ζ
|
79
|
Mizar (
Mizari
)
|
2,23
|
78
|
A2 V
|
β
|
48
|
Merak (
Maraki
)
|
2,34
|
79
|
A1 V
|
γ
|
64
|
Phekda (
Fahidhi
)
|
2,41
|
84
|
A0 V SB
|
ψ
|
52
|
|
3,00
|
147
|
K1 III
|
μ
|
34
|
Tania Australis
|
3,06
|
ca. 230
|
M0 III
|
δ
|
69
|
Megrez
|
3,32
|
81
|
A3 V
|
Tanbihi
- ↑
Uhusika milikishi
(
en:genitive
)
ya "Ursa Major" katika lugha ya
Kilatini
ni "Ursae Majoris" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Ursae Majorise, nk.
- ↑
ling. Knappert 1993
- ↑
The Constellations
, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
- ↑
"The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922
, iliangaliwa Mei 2017
- ↑
Stars: "Alioth"
, tovuti ya Prof Jim Kaler, Chuo Kikuu cha Illinois
- ↑
Star Tales: Dubhe
, tovuti ya Prof Jim Kaler
Viungo vya Nje
Marejeo
- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 63 ff (
online hapa kwenye archive.org
)
- Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331