Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Donato di Niccolo di Betto Bardi
(*
1386
hadi
13 Desemba
1466
) huitwa kwa kawaida
Donatello
(Donato mdogo) alikuwa
msanii
wa
zama ya mwamko
nchini
Italia
.
Alikuwa mwenyeji wa mji wa
Firenze
akawa
mchongaji
mashuhuri wa wakati wake.
Donatello alizaliwa Firenze kama mtoto wa fundi wa kuchanua sufi Niccolo di Betto Bardi. Mwaka
1401
alianza kazi kama msaidizi wa mchongaji na fundi shahabu
Lorenzo Ghiberti
. Inasemekana alisafiri
Roma
na kutazama
sanamu
za
Waroma wa Kale
.
Tangu
1407
alionekana kama fundi na mchongaji wa kujitegemea aliyepewa kazi ya kupamba ma
kanisa
na majumba ya matajiri. Alionyesha ya kwamba alijifunza mengi kutoka
sanaa
ya Waroma wa Kale hivyo alikuwa kiongozi wa harakati ya mwamko wa sanaa ya kale katika Italia iliyoathiri sanaa kote
Ulaya
.
Donatello alitumia
ubao
,
marumaru
na
metali
kwa kazi zake.
Kati ya sanamu zake mashuhuri sana ni
Daudi kama mchungaji kijana
na
Maria Magdalena
.
-
Sanamu ya Daudi
-
-
Jenerali Gattamelata
-
-
-
Juditi
na Holofernes (Palazzo Vecchio - Firenze)
-
|
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Donatello
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|