Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
,
Dolar
(pia
dola
,
Kiing.
dollar
) ni jina la
pesa
ya
Marekani
na nchi mbalimbali duniani.
Dola ya Marekani
au
US-Dollar
ndiyo inayojulikana zaidi, lakini kuna nchi zaidi ya 20 zinazotumia neno "Dollar" kwa pesa yao.
Nchi zenye pesa inayoitwa "Dollar" (dola)
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Asili ya jina hilo ni
neno
la
Kijerumani
"taler" (au: thaler) kwa ajili ya
sarafu
ya
fedha
iliyotolewa kwenye
mji
wa
Joachimsthal
kule
Bohemia
(
Ucheki
) mnamo mwaka
1518
.
Wakati ule
migodi
ya Joachimsthal ilikuwa na fedha nyingi kiasi kwamba mji ulianza kutoa pesa zake. Pesa hizo zilitwa (kufuatana na mji) "Joachimsthaler", iliyofupishwa kuwa "taler" tu.
Taler ilikuwa pesa iliyopendwa sana
Ulaya
ikasambaa kote.
Hispania
ilitumia jina hilo kwa "dolaro" yake kuanzia mwaka
1575
. Dolaro ya Hispania ilikuwa baadaye pesa ya kisheria ya Marekani ilipojitenga na
Uingereza
na kuanzisha pesa yake mwaka
1792
.