UDOM.
Chuo Kikuu cha Dodoma
(
kifupisho
chake ni UDOM) ni
chuo kikuu
ambacho bado kinajengwa
mjini
Dodoma
,
Tanzania
.
Ujenzi
unafanyika katika kipande cha
ardhi
cha
hekta
6,000 karibu na Dodoma,
kilomita
400
magharibi
kutoka
jiji
la
Dar es Salaam
na kilomita 7 kutoka Dodoma mjini.
Mafunzo yalianza rasmi septemba
mwaka
2007
, wakati
wanafunzi
zaidi , walijiunga na
programu
zilizotolewa katika
vitivo
vya Humanities, Sayansi ya Ujamaa, Elimu na 'Informatics and Virtual Education'(Elimu angavu). Vyuo vya Sayansi ya Maisha na Afya na Sayansi zinazolingana zilianzishwa mwaka.Hivi sasa UDOM ndicho chuo kikuu kinachokuwa kwa kasi nchini, ni kikubwa kuliko chuo kikuu chochote ndani ya nchi, na kinasifiwa kwa kutoa watahiniwa wenye uwezo na uwezo wa kushindana katika soko la ajira.
Sambamba na Maono ya Nchi ya Maendeleo ya 2025, Chuo Kikuu cha Dodoma, kikishamalizika kamili, kitaweza kuwachukua wanafunzi 40,000 katika
taaluma
mbalimbali. Hii ni zaidi ya mara
mbili
ya ukubwa wa sasa wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
. Hata hivyo, chuo kikuu cha Dodoma bado kipo katika maendeleo.
[1]
Kilitangazwa kuwa chuo
namba
mbili
(2) kwa
ubora
wa
elimu
nchini Tanzania mnamo
Machi
2018
, kikitanguliwa tu na
chuo kikuu cha Dar es Salaam
.Mpaka mwwaka 2018 chuo kikuu cha Dodoma kilikuwa na vitivo saba, vikiwa na insia zenye kozi tofautitofauti.
Chuo kikuu cha Dodoma kwa sasa kina ndaki saba: Ndaki ya Sayansi ya Ardhi, Ndaki ya Sayansi Asilia na
Hisabati
, Ndaki ya Informatics na Virtual Education(Elimu angavu), Ndaki ya
Elimu
, Ndaki ya
Binadamu
na
Sayansi
ya
Jamii
, Ndaki ya
Afya
na Sayansi Shirikishi na Ndaki ya Mafunzo ya
Biashara
na
Sheria
, hivi karibuni pia kumeanzishwa ndaki mpya za kitaaluma ndani ya Ndaki ya Binadamu na
Sayansi ya Jamii
UDOM kilichopewa jina la
Taasisi
ya Masomo ya Maendeleo (IDS) chenye jukumu la kuimarisha wataalamu ndani ya fani ya Masomo ya Maendeleo.
Chuo hiki kikuu hutoa programu mbali mbali za
shahada ya kwanza
na wahitimu kutoka karibu nyanja zote za
maarifa
.
Katika Ndaki ya elimu, programu kadhaa za shahada ya kwanza hutolewa kwa kuzingatia masuala yanayoikabili sekta ya elimu nchini
Tanzania
na nje ya nchi. Kuna
digrii
11 tofauti za bachela katika chuo cha elimu.
Ndaki ya Elimu angavu (Informatics and Virtual Education) inajulikana sana kwa umahiri wake katika fani ya
Tehama
nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.Ndaki hii inatoa programu za shahada ya kwanza na
uzamili
katika maeneo kama vile
sayansi ya kompyuta
,
uhandisi
wa kompyuta, uhandisi wa mawasiliano ya
simu
, usalama wa habari, mifumo ya taarifa za afya na biashara na programu nyinginezo nyingi.
- ↑
"SARUA"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2011-07-28
. Iliwekwa mnamo
2009-12-23
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Chuo Kikuu cha Dodoma
kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|