Chuo Kikuu
ni
taasisi
ya
elimu
ya ngazi ya juu ambako wanafunzi wanafundishwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao hufundisha pamoja na kuendesha
uchunguzi
wa elimu mpya.
Wanafunzi husoma kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kupata elimu hadi kupita mitihani ya
shahada
au digrii kama vile ya
bachelor
(ya kwanza), ya
uzamili (master)
(ya pili) na ya
uzamivu, PhD
(ya tatu).
Siku hizi chuo kikuu kinatakiwa kuwa na sifa kadhaa za kukitofautisha na vyuo au taasisi nyingine kama vile:
- kuunganisha fani mbalimbali kwa kukitofautisha na vyuo vinavyofundisha fani moja tu; kwa mfano chuo cha
ualimu
, chuo cha
teolojia
, chuo cha
uganga
. Hata hivyo kuna vyuo vikuu vinavyokazia na kufundisha hasa upande mmoja wa elimu
- kuunganisha kazi ya kufundisha na kazi ya uchunguzi kwa kukitofautisha na taasisi za uchunguzi zisizolenga mafundisho ya wanafunzi wa kawaida isipokuwa kuna nafasi ya kupata udokta
- kutoa mafundisho ya ngazi ya juu inayokubaliwa kimataifa
- kwa kawaida chuo kikuu kinatakiwa na kiwango kikubwa cha kujitawala na
uhuru wa taaluma
. Hali halisi hii inategemea
mazingira
: kuna tofauti kubwa kati nchi na nchi. Kufaulu katika maendeleo ya uchunguzi kunahitaji uhuru wa kuangalia, kuelewa na kujadili mawazo na
fikra
kutoka pande zote za
dunia
hata kama mawazo kadhaa hayakubaliwi katika mfumo wa kisiasa au kijamii ya nchi yenyewe.
Jamii
katika tamaduni mbalimbali zilianzisha taasisi maalumu kwa elimu ya ngazi ya juu. Kati ya vyuo vya kwanza vinayofanana kiasi na chuo kikuu cha kisasa kuna hasa taasisi katika
Uhindi
,
Ugiriki ya Kale
,
Uajemi
,
Ulaya
na nchi za Kiislamu.
Mfumo wa kufundisha na kuratibu elimu ulio msingi wa vyuo vikuu vya kisasa ulianza hasa katika Ulaya ya
karne za kati
.
Vyuo hivi vya Ulaya viliendelea kuwa mahali pa
maendeleo
na kukuza
sayansi
ya kisasa. Kutoka hapa mfumo wa chuo kikuu pamoja na utaratibu wa ngazi zake za elimu ulisambaa kote duniani.
Kitovu cha kwanza cha elimu ya hali ya juu barani
Afrika
kilikuwa
maktaba ya Aleksandria
nchini
Misri
lakini ilikuwa taasisi ya kukusanya vitabu na mahali pa uchunguzi, si mafundisho.
Kihistoria vyuo vya kwanza vilivyotoa mafundisho kwenye hali ya juu ya kimataifa ya wakati wake vilikuwa chuo cha
Al-Karaouine
mjini
Fes
,
Moroko
tangu mwaka
859
BK na
Al Azhar
mjini
Kairo
,
Misri
tangu mwaka
975
.
Upande wa kusini kwa Sahara ni
Madrasa ya Sankore
mjini
Timbuktu
(
Mali
) iliyotoa mafundisho ya hali ya juu kuanzia takriban mwaka
1400
.
Vyuo vikuu vya kisasa vilianzishwa na
wamisionari
katika
karne ya 19
nchini
Sierra Leone
na
Afrika Kusini
; vilianzishwa kama vyuo vya ualimu na kuendelea kuwa vyuo vikuu kamili.
Chuo Kikuu cha kwanza katika
Afrika ya Mashariki
kilikuwa
Chuo Kikuu cha Makerere
ambacho ni chuo mama cha vyuo vya
Nairobi
na
Dar es Salaam
.
Siku hizi ni hasa vyuo vikuu vya Afrika Kusini vinavyothaminiwa kuwa bora katika bara la Afrika.
Orodha ya utathmini wa vyuo vikuu bora barani Afrika kwa mwaka
2013
ilikuwa kama ifuatayo:
- University of South Africa
,
Afrika Kusini
- University of Cape Town
, Afrika Kusini
- Universiteit Stellenbosch
, Afrika Kusini
- Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
,
Tanzania
- University of KwaZulu-Natal
, Afrika Kusini
- University of Pretoria
, Afrika Kusini
- Chuo Kikuu cha Kairo
,
Misri
- University of the Witwatersrand
, Afrika Kusini
- University of the Western Cape
, Afrika Kusini
- Obafemi Awolowo University
,
Nigeria
- Makerere University
,
Uganda
- University of Botswana
,
Botswana
Kufikia mwaka 2016, vyuo vikuu kumi bora ni vyote vya Afrika Kusini. Cha Dar es Salaam kimekuwa cha 26.
[1]