Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christiaan Huygens
(14 Aprili 1629 ? 8 Julai 1695) alikuwa mtaalamu wa
fizikia
,
hisabati
na
astronomia
kutoka nchini
Uholanzi
aliyezaliwa mjini
Den Haag
.
Alizaliwa kama mtoto wa Constantijn Huygens aliyekuwa mshairi mashuhuri wa Uholanzi. Hivyo kupitia babake alipata kujua watu maarufu kama vile
Rembrandt
,
Peter Paul Rubens
na
Rene Descartes
. Alipokuwa mdogo alifundishwa na baba akaendelea kusoma sheria kwenye chuo kikuu cha Leiden baadaye akahamia masomo ya
hisabati
na
sayansi
.
Alikuwa kati ya watu wa kwanza waliofikiri ya kwamba nuru ina tabia ya wimbi. Kutokana na nadharia yake juu ya tabia za nuru aliweza kuboresha umbo la
lenzi
. Mwaka 1655 alitengeneza
darubini
iliyoboreshwa na kuchungulia sayari ya
Zohali
(Saturnus). Alitambua mwezi wa
Titan
na mwaka uliofuata aliweza kutangaza ya kwamba bangili za Zohali zinafanywa kwa miamba.
Alibuni pia saa makini kushinda saa nyingine za
wakati wake
.
Chombo cha angani
Cassini?Huygens
kimepokea jina lake kwa heshima ya Huygens pamoja na Mwitalia
Giovanni Domenico Cassini
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: