Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chombo cha usafiri
ni
kifaa
chochote kinachotumiwa kusafirisha
watu
au
mizigo
.
Vyombo vya usafiri hutofautiana kama vinahudumia
usafiri
wa
nchi kavu
, wa
majini
au wa
hewani
.
Mifano ni
Hutofautishwa pia kama vinalenga matumizi ya watu binafsi au matumizi ya
umma
.
- Baisikeli, pikipiki na motokaa mara nyingi hutumiwa na wenye chombo hiki cha usafiri. Lakini zinaweza kutumiwa pia kama sehemu ya
usafiri wa umma
kwa mfano gari kama
teksi
au baisikeli kama
boda-boda
. Magari makubwa na mazito kama
lori
husafirisha mizigo.
- Treni,
reli
ya mjini,
metro
na
mabasi
ni vyombo vya
usafiri
wa umma kwenye nchi kavu.
- Meli na
feri
ni vyombo vya usafiri wa umma majini, lakini boti ndogo mara nyingi hutumiwa na watu binafsi. Isipokuwa kuna
miji
kando ya
mto
au
bandarini
penye
huduma
ya teksi ya maji kwa kutumia boti dogo.
Meli ya mizigo
husafirisha
bidhaa
.
- Eropleni
ndogo hutumiwa na watu binafsi ilhali
matajiri
wachache ni wenye ndege kubwa. Kwa kawaida ndege kubwa hubeba abiria kama vyombo vya usafiri wa umma. Eropleni ndogo zinapatikana pia kama teksi ya hewani.