Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Charles Messier
(
tamkaː sharl mesyee
;
26 Juni
1730
?
12 Aprili
1817
) alikuwa
mwanaastronomia
kutoka nchini
Ufaransa
anayekumbukwa kwa kutunga orodha ya
magimba ya angani
iliyojulikana kwa
jina
la "
Orodha ya Messier
".
Namba
za orodha yake zinatumiwa hadi leo kwa kutaja magimba ya angani mbalimbali, kwa mfano “M31” ambayo ni
Galaksi ya Andromeda
.
Maisha
Alizaliwa katika jimbo la
Lorraine
, Ufaransa. Alianza kuvutiwa na habari za
astronomia
baada ya kuona
nyotamkia
kubwa ya
mwaka
1744
na
kupatwa kwa jua
mnamo
tarehe
25 Julai
1748
.
Kazi
yake ya kwanza kuanzia mwaka
1754
ilikuwa
ajira
kama
karani
wa
Joseph Nicolas Delisle
aliyekuwa mwanastronomia
mkuu wa jeshi
la maji
la Ufaransa. Kazi ya Messier ilikuwa pamoja na kuchora
ramani
. Deslisle alitambua uwezo wake alimfundisha pia misingi ya
astronomia
. Hasa alimfundisha kuandika kila
kitu
alichotazama
angani
pamoja na maelezo yakinifu.
Mwaka
1757
aliagizwa na Delisle kutafuta
Kometi ya Halley
iliyotabiriwa kurudi mwaka ule; aliitambua tu kwenye
Januari
1759
kwa sababu
utabiri
ulikuwa na makosa. Mwaka
1761
alitazama
mpito wa Zuhura mbele ya jua
na mwaka
1764
alifaulu kukuta nyotamkia ya kwanza isiyojulikana bado.
Tangu 1764 Messier alitafuta hasa nyotamkia angani. Kwa jumla alizitambua 13:
[1]
- C/1760 B1 (Messier)
- C/1763 S1 (Messier)
- C/1764 A1 (Messier)
- C/1766 E1 (Messier)
- C/1769 P1 (Messier)
- D/1770 L1
(Lexell)
- C/1771 G1 (Messier)
- C/1773 T1 (Messier)
- C/1780 U2 (Messier)
- C/1788 W1 (Messier)
- C/1793 S2 (Messier)
- C/1798 G1 (Messier)
- C/1785 A1 (Messier-
Mechain
)
Pamoja na nyotamkia hizi alikuta pia kiasi cha magimba mengine kama vile
nebula
,
fungunyota
au
galaksi
.
Tangu mwaka
1771
alianza kuzipeleka kwenye
umma
kwa njia ya orodha yake alimoorodhesha magimba 110 zinazotajwa hadi leo kwa namba kama “Messier-1” (au M1) na kadhalika
[2]
.
Tazama pia
Marejeo
- ↑
"Maik Meyer. Catalog of comet discoveries"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2008-07-16
. Iliwekwa mnamo
2017-04-24
.
- ↑
History of the Messier Catalogue
, tovuti ya
http://www.messier.seds.org/
"The Messier catalogue", iliangaliwa Machi 2019
Viungo vya Nje