Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brazzaville
ni
mji mkuu
wa
Jamhuri ya Kongo
. Una wakazi 2,308,000 (
mwaka
2019
) ambao ni sawa na 40
%
ya wananchi wote.
Uko kando ya
mto Kongo
ukitazamana na
mji
wa
Kinshasa
ng'ambo ya
mto
.
Brazzaville una
bandari
kwenye mto Kongo na mwanzo wa
reli
kuelekea
pwani
.
Jina
la Brazzaville limetokana na
Mfaransa
Pierre Savorgnan de Brazza
aliyenunua hapa ardhi kutoka kwa
chifu
Makoko
na kujenga kituo kilichokua na kuwa mji baadaye.
Tangu mwaka
1898
Brazzaville ulikuwa mji mkuu wa
Kongo ya Kifaransa
ukawa na wakazi 5,000 mnamo
1900
walioongezeka kuwa
lakhi
moja mwaka
1950
.
Mwaka
1940
Brazzaville ulikuwa kwa muda mfupi mji mkuu wa
Ufaransa Huru
yaani
Ufaransa
usio chini ya
Ujerumani
hadi kuhamia kwa
serikali
hiyo kwenda
Algiers
.