Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Tajikistan
imepatikana tangu mwaka
1992
yaani mwaka mmoja baada ya uhuru wa
Tajikistan
.
Ina milia mitatu ya nyekundu, nyeupe na kijani. Mlia mweupe ni pana kuliko milia mingine. Katikati kuna alama ya rangi dhahabu ya taji lenye nyota saba.
Rangi za bendera ni sawa na rangi za bendera ya
Uajemi
. Utamaduni na lugha za nchi hizi mbili ni karibu sana.