Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa beatboxing ya kisasa
Biz Markie
akifanya beatboxing
D.R.E.S. akifanya beatboxing huko mjini Atlanta
Beatboxing
ni jina la kutaja aina ya upigaji ngoma kwa kutumia mdomo - hasa kwa kuhusisha sanaa ya utayarishaji wa midundo ya ngoma,
wizani
, na sauti za kimuziki kwa kutumia mdomo wa mtu, midomo, ulimi, na sauti. Pia inaweza kuhusisha kuimba, sauti za mwigo wa hali ya turntable, na pia uigaji wa honi, nyuzi za gitaa, na vyombo vingine vya muziki. Leo hii beatboxing inahusiana na
utamaduni wa hip-hop
, ikiwa kama moja kati ya "elementi" zake, ijapokuwa mwisho wake si
muziki wa hip hop
tu.
[1]
[2]
Mkali wa kupiga beatboxing kwa sana ni
Michael Winslow
kutoka katika filamu ya
Police Academy
.