Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Aktiki
(Aktika) ni bahari inayozunguka
ncha ya kaskazini
. Ni sehemu ya eneo la
Aktiki
. Wataalamu wengine huitazama kama
bahari
ya pekee lakini wengine huona ni
bahari ya pembeni
ya
Atlantiki
. Kina kikubwa kiko karibu na visiwa vya
Spitzbergen
chenye mita 5,608.
Bahari ya Aktiki iko kati ya pwani za
Asia
ya Kaskazini,
Alaska
na
Kanada
katika
Amerika ya Kaskazini
,
Greenland
na
Skandinavia
(
Ulaya
). Eneo lake ni 14.056
km²
. Kati ya Greenland na Skandinavia kuna uwazi kubwa unaojifungua kwa Atlantiki ya Kaskazini na
mlango wa Bering
unaunganisha bahari hii na
Pasifiki
.
Sehemu kubwa ya eneo lake hufunikwa na
barafu
yenye unene wa mita 3 lakini sehemu hii imeanza kupungua kutokana na
kupanda kwa halijoto duniani
.
Mito muhimu inayoingia ni
Ob
,
Yenissei
,
Lena
na
Kolyma
upande wa
Siberia
(
Urusi
) halafu mito ya
Yukon
na
Mackenzie
upande wa Amerika ya Kaskazini.
|
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
|