Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Antonio Manuel de Oliveira Guterres
(alizaliwa
30 Aprili
1949
) ni
mwanasiasa
wa
Ureno
ambaye anatumikia kama
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
tangu
mwaka
2017
. Hapo awali, alikuwa
Kamishna
wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) kati ya 2005 na 2015.
Guterres alikuwa Waziri Mkuu wa Ureno kutoka 1995 hadi 2002 na alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kisoshalistu cha Ureano kutoka 1992 hadi 2002. Alihudumu kama Rais wa Umoja wa Vyama vya Kisoshalisti Duniani kutoka 1999 hadi 2005.
Katika kura ya kupima mawazo kwenye miaka 2012 na 2014 wananchi wengi wa Ureno walimtaja mara mbili alikuwa waziri mkuu bora wa nchi hii anayekumbukwa.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: