Angahewa
ni matabaka ya
gesi
za
hewa
yanayozingira
sayari
au
gimba lingine la angani
yakishikwa na
uvutano
wa gimba husika.
Angahewa ya Dunia
Angahewa inakinga
uhai
duniani
kwa kupunguza
mnururisho
wa
urujuanimno
wa
Jua
, kutunza
halijoto
duniani kwa kuakisisha
mawimbi
ya
mialekundu
, kupunguza tofauti kati ya
baridi
na
joto
na kuwapa
wanyama
na
mimea
viwango vya
oksijeni
na
nitrojeni
wanavyohitaji.
Magimba ya angani mengine kama
sayari
au Jua huwa pia na aina za angahewa ingawa gesi zake ni tofauti na za duniani.
Gesi zilizopo katika angahewa ya Dunia ni hasa
nitrojeni
(78
%
) na
oksijeni
(21%) pamoja na viwango vidogo lakini muhimu vya
arigoni
(0.9%),
dioksidi kabonia
(0.035%),
mvuke
wa
maji
na gesi nyingine mbalimbali.
Angahewa haina mwisho kamili, ila inazidi kuwa hafifu jinsi inavyofikia juu.
Asilimia
75 za
masi
ya hewa yake iko katika
angavungu
hadi
kilomita
11 juu ya uso wa Dunia.
Uzito
wa hewa hupimwa kama
kanieneo angahewa
.
Halijoto na matabaka ya angahewa
Sehemu za angahewa zina baridi au joto zaidi kutegemeana na
kimo
. Tukipaa juu ya uso wa Dunia halijoto inazidi kuwa baridi, baadaye joto tena, kadiri jinsi tunavyopaa. Mabadiliko ya halijoto yanafuata muundo wa tabaka zinazotofautishwa na kiwango cha joto au baridi kinachopimwa.
Kwa jumla inawezekana kutofautisha matabaka 5 ambayo ni
- Angavurugu
(troposphere) - inaanza kwenye uso wa Dunia na kuishia mnamo kilomita 7 (juu ya ncha za Dunia) - 15 (juu ya sehemu za
tropiki
) juu yake; baridi inazidi jinsi unavyopaa juu (kwa hiyo ni baridi mlimani kushinda chini); mawingu yako hapa na hii ni tabaka ambako
halihewa
inatokea.
- Angatando
(stratosphere) - inaishia kwenyi kimo cha
km
50; hapa joto linaanza kuzidi tena.
Eropleni
kubwa zinapita hapa kwa sababu hakuna upepo mwenye nguvu inayosumbua mwendo
- Angakati
(mesosphere) - inaishia kwa kimo cha km 80 - 85; hapa baridi inazidi jinsi unavyopaa; kuna upepo mkali.
- Angajoto
(thermosphere) - inaishia kwa kimo cha km 500 - 600; joto linapanda pamoja kimo; tabaka hii ni muhimu kwa mawasiliano ya redio kwa sababu inaakisisha miale ya redio ya AM.
- Angajuu
(exosphere) - ni tabaka la nje inayoanza kati ya km 500 - 1000 na kuwa hafifu kadri unayopaa juu zaidi; inafikia kilomita maelfu hadi kwa kimo cha takriban 10,000 km ambako hewa haipimiki tena
Matabaka ya juu, yaani tabakajoto na tabakanje, huitwa pia
angaioni
kwa sababu
atomu
za gesi zake zinapatikana katika hali ya
ioni
zilizopoteza
elektroni
kutokana na kupigwa na miale ya Jua iliyo bado kali sana hapo nje.
Angahewa kwenye sayari
Nje ya Dunia yetu angahewa imetambuliwa pia kwenye
sayari
nyingine. Katika
Mfumo wa Jua
kuna sayari 4 za ndani zinazofanana kiasi, ni
Utaridi
,
Zuhura
, Dunia na
Mirihi
. Zote nne ni sayari zinazofanywa na
mwamba
.
- Kati ya hizi Utaridi haina angahewa, ikiaminiwa yote imepotea kutokana na kupigwa vikali na
upepo wa Jua
lililo karibu na sayari hii.
- Zuhura ina angahewa nzito, hasa ya
dioksidi kabonia
(CO
2
)
- Mirihi
na angahewa hafifu sana ya dioksidi kabonia (CO
2
). Inaaminiwa kuwa imepotea asilimia kubwa ya angahewa yake. Mirihi haina
uga sumaku
na hivyo upepo wa Jua unapiga sayari hii moja kwa moja na kusukuma
molekyuli
za angahewa mbali kwenda
anga-nje
.
Sayari kubwa za nje kama
Mshtarii
na
Zohari
si rahisi vile kuofautisha kati ya sayari yenyewe na angahewa yake. Sayari hizi huitwa pia "jitu za gesi" kwa sababu asilimia kubwa ya sayari yote ni elementi kama
hidrojeni
na
heli
ambazo kwetu duniani zinapatikana kama gesi. Kutokana na umbali mkubwa na Jua ni baridi zaidi hadi gesi hizi kupitia katika hali mango. Vilevile hidrojeni katika kiini cha Mshtarii inaaminiwa kuwa katika hali metalia kutokana na shinikizo kubwa ya masi yake.
Kuna miezi kadhaa zinazunguka sayari za Jua ambako angahewa zimegundliwa, kwa mfano kwa mwezi
Titani
wa Zohali na miezi ya
Europa
na
Ganimedi
ya Mshtarii.
Viungo vya Nje