Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa
(kwa
Kiingereza
: International Phonetic Alphabet, kifupi
IPA
) ni mfumo wa
alfabeti
unaolenga kuonyesha
sauti
za
lugha
zote
duniani
. Imetungwa na
wataalamu
wa
isimu
wanaoshirikiana katika
Shirika la Kimataifa la Fonetiki
(International Phonetic Association). Inatumiwa na watunga
kamusi
,
walimu
na
wanafunzi
wa lugha za kigeni,
wanaisimu
na wafasiri kote duniani. Kwa hiyo tunakuta
alama
zake katika kamusi na mara nyingi pia kwenye makala za
Wikipedia
.
Msingi wa IPA ni
alfabeti ya Kilatini
pamoja na
herufi
za pekee zilizochukuliwa kutoka alfabeti nyingine. Herufi hizo zinaunganishwa na alama za pekee.
Mfano ni alama zinazoonyesha sauti tofauti ambazo mara nyingi zinaonyeshwa kwa herufi "
A
" ambazo zinaweza kuwa na sauti tofauti katika lugha na
lahaja
mbalimbali kama vile a
▶
?
, ?
▶
?
, ?
▶
?
, ?
▶
?
, æ
▶
?
, ?? au ?
▶
?
(bofya
pembetatu
ndogo kwa kusikia sauti)
.
Orodha ya alama zote za IPA pamoja na sauti inapatikana katika Wikipedia ya Kijerumani hapa
de:Liste_der_IPA-Zeichen
Tangu masahihisho ya
mwaka
2005
[1]
kuna herufi 107 na alama za pekee 56.
- ↑
"IPA: Alphabet". Langsci.ucl.ac.uk. Archived from the original on 10 October 2012. Retrieved 20 November 2012.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
lugha
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa
kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|