Albert Szent-Gyorgyi ( 16 Septemba 1893 ? 22 Oktoba 1986 ) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Hungaria . Pamoja na nchi yake ya kuzaliwa alifanya kazi katika nchi mbalimbali kama Uholanzi, Ujerumani, Uingereza na Marekani. Alichunguza mambo mengi ya biokemia, na anajulikana hasa kwa utafiti wake wa vitamini C . Mwaka wa 1937 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba .