Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ala ya muziki
ni
kifaa
kinachotoa
sauti
zinazotumiwa katika
muziki
. Kila ala ya muziki inatoa mitetemo katika
hewa
inayoendelea kusambaa na kupokewa na
masikio
kama sauti.
Kimsingi kila
kitu
kinachotoa sauti kinaweza kutumiwa kama ala ya muziki, lakini kwa kawaida
jina
hili linatumika kwa vitu vilivyotengenezwa hasa kwa shabaha hii. Wakati mwingine hata sauti ya
binadamu
inatajwa kama ala ya muziki.
Kuna aina nyingi za ala za muziki. Mara nyingi zinaainishwa na kutajwa kutokana na mbinu zake za kutoa sauti:
- ala za mitemo (kwa
Kiingereza
idiophone
) ambako ala yote inatetema, kama vile
kengele
,
mafurungu
,
marimba
- ala za nyuzi (ing.
chordophone
) kama vile
gitaa
,
fidla
,
selo
,
zeze
au
piano
; hapa uzi au waya iliyokazwa inapigwa au kuchuliwa hivyo inaanza kutetema
- ala za utando (ing.
membranophone
) kama vile
ngoma
, tari, hapa utando inatoa mitetemo ikipigwa
- ala za hewa (ing.
aerophone
) ambako nguzo ya hewa inatetemewa, mfano
filimbi
,
kinanda cha filimbi
,
zumari
,
kipenga
,
baragumu
, au
tarumbeta
. Katika kundi hili hewa inaweza kupititishwa kwenye kona kali kama kwa filimbi, au kwa kipande cha tete inayotetema katika mwendo wa hewa, au kwa kutumia midomo kama asili ya mitetemo kama kwenye tarumbeta.
- katika
karne ya 20
zilibuniwa ala za
muziki elektroniki
ambazo zinatoa sauti kupitia
kipaza sauti
.
Wengine hutofautisha ala za muziki kutokana na namna ya matumizi, kama vile kupiga, kupuliza hewa, kupiga vibanzi au funguo (
keyboard
), kuchulia waya.
Kila jamii na kila
utamaduni
kwenye
dunia
imewahi kubuni ala zake za pekee.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ala ya muziki
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|