Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akina Grimm
(
Jer.
:
Die Bruder Grimm
, pia
Gebruder Grimm
;
ing.
"Brothers Grimm") ni namna ya kutaja kwa pamoja wataalamu na ndugu kaka
Jakob Grimm
na mdogo wake
Wilhelm Grimm
. Wamekuwa mashuhuri hasa kwa kukusanya hekaya,
ngano
na hadithi nyingine za Ujerumani na kuzilinganisha na masimulizi kutoka nchi nyingine. Wanahesabiwa kati ya waanzilishaji wa fani ya
isimu
au sayansi ya lugha.
Katika Ujerumani na kwa wataalamu wa
lugha za Kigermanik
wanajulikana pia kwa kuanzisha kazi ya kamusi kubwa ya lugha ya Kijerumani inayoendelea kuhaririwa hadi leo na kufikia vitabu 32.
Mkusanyiko wao wa ngano unasomwa hadi leo hii. Kwa kazi hii walitembelea vijiji vingi na kuandika hekaya na ngano jinsi zilivyosimuliwa na wazee (
Grimms Marchen
).
Kati ya ngano walizokusanya ni
Mweupe Theluji
("Schneewittchen"), "Sinderella" "(Aschenputtel)", "Hansel na Gretel" ("Hansel und Gretel") na takriban 200 mengine.
Kigezo:Wikiquote-en
Wikimedia Commons ina media kuhusu: