Adolf Friedrich Johann Butenandt ( 24 Machi 1903 ? 18 Januari 1995 ) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani . Hasa alichunguza homoni zisababishazo kuvutiwa kijinsia. Mwaka wa 1939 , pamoja na Leopold Ruzicka alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia . Serikali ya Ujerumani walimlazimisha kukataa tuzo lakini aliruhusiwa kuipokea mwaka wa 1949.