Mwandishi
kwa maana ya kimsingi ni
mtu
anayeandika.
Jina
hilo linaweza kumtaja
mtu
aliyeweka matini kwenye
karatasi
tunayosoma. Linaweza pia kumtaja
mtungaji
wa
andiko
hata kama hatuna uhakika kama aliliandika mwenyewe kwa
mkono
wake, kwa hiyo ni karibu na maana ya "mtungaji".
Tangu uenezaji wa
elimu
ya
shule
kwa watu wengi tendo la kuandika si jambo la ajabu tena. Lakini kwa kipindi kirefu cha
historia
ya
binadamu
walikuwepo watu wachache tu waliojua kusoma na kuandika na kwa vipindi vile
kazi
ya "mwandishi" ilikuwa muhimu katika
jamii
.
Kubuni uwezo wa kutunza habari kwa
alama
ya kimaandishi kulikuwa
maendeleo
makubwa katika historia ya binadamu. Chanzo cha
maandishi
kilikuwa katika kutunza
kumbukumbu
ya
kodi
na
mapato
.
Watawala
wa kwanza waliweza kushika hivi ni kiasi gani cha
nafaka
au
mifugo
kinachochangiwa na
kijiji
au
mkoa
fulani.
Kutunza kumbukumbu hii kulihitaji watu waliojua kutumia alama gani kwa maana gani na walioweza kuzitambua tena baada ya
muda
. Watu hao walikuwa waandishi wa kwanza. Kulingana na maendeleo ya
mwandiko
idadi ya alama iliongezeka zilizotaja pia mambo yasiyoonekana kama dhana za kijamii au
kidini
.
Waandishi walikuwa mara nyingi
maafisa
wa
mfalme
au mtawala waliokuwa karibu naye kwa sababu elimu yao ilikuwa muhimu kwa utawala. Tangu uenezaji wa
biashara
wafanyabiashara
walitumia pia maandishi, hivyo walijifunza wenyewe kuandika au waliajiri waandishi.
Katika eneo la
Mesopotamia
walimwabudu
mungu
mlinzi wa waandishi kwa jina
Nabu
. Katika
maktaba
ya
matofali ya kikabari
ya
Niniveh
kuna matini inayosifu kazi ya mwandishi: "Onyesha bidii katika
sanaa
ya kuandika, maana itakupatia
utajiri
kwa wingi"
[1]
Katika
Misri ya Kale
kazi ya mwandishi iliheshimiwa sana. Waandishi walionyeshwa mara nyingi kwa sanamu za kuchongwa zilizohifadhiwa hadi leo. Mwandishi
Imhotep
aliyekuwa afisa mtendaji mkuu wa
farao
Djoser
alipewa
heshima
ya kimungu baada ya
kifo
chake.
[2]
Wana wa waandishi walifundishwa katika
nyumba
za
baba
halafu kupelekwa shule wakaingia katika huduma ya
serikali
na wakati mwingine kurithi nafasi ya baba.
[3]
Hao waandishi walitimiza shughuli zinazotekelezwa leo na
karani
,
mhasibu
au
katibu
.
Katika
Agano la Kale
"mwandishi" alikuwa mtu aliyenakili
sheria
ya
Mungu
kwa watu waliotaka kuisoma, lakini baada ya
uhamisho wa Babeli
alizidi kuwa mtu wa maana kama
mtaalamu
ambaye uamuzi wake katika mambo ya
dini
uliheshimiwa sana. Katika miaka ya baadaye tena waandishi walizidi kupata nguvu na ushawishi katika Israeli, wakati ambapo
manabii
walipungua kwa
idadi
na umuhimu.
Kando na kuandika, waandishi wa leo wana vipawa vingine tofauti kama vile kuigiza, kuripoti katika vyombo vya habari na kusanii kwa sauti (voice artists) kama vile Raheel Farooq. Kando na kuandika vitabu vya chapa waandishi mamboleo wanafanya vitabu elektroniki yaani ebooks. Wengine waandika kwa wavuti zao. Kati ya waandishi bingwa hapa Afrika wa mambo leo ni kama
Wallah bin Wallah
,
Mohamed Said
,
Ken Walibora
na
Yericko Y. Nyerere
.
Kuna waandishi wengine ambao kazi yao ni kuwaandikia wengine. Katika dunia ya leo, ambayo kazi nyingi zafanyika kwa mtandao, waandishi hao huenda wakapewa kazi ya kuwafanyia wengine maandishi ya wavuti zao (freelance website content writers) au kuwafanyia maandishi waliyopewa chuoni.
Kabla ya kupatikana kwa
uchapaji
njia pekee ya kupata nakala za
hati
,
sheria
, matangazo na
vitabu
ilikuwa kunakili matini hizi kwa mkono. Jamii zilizoendelea katika historia zilikuwa na maelfu ya watu ambao kazi yao ilikuwa kunakili matini hizi. Walipatikana katika ofisi za serikali, ofisi za shirika za biashara, taasisi za elimu au pia kama waandishi waliojitegemea na kufanya kazi yao kibarua.
Kazi yao ilipotea kwa kiasi kikubwa tangu kupatikana kwa
uchapaji
. Hadi leo katika nchi zenye watu wengi wasiojua kusoma kuna waandishi wanaofanya kazi hii kwa wengine. Kazi yao ni zaidi kuandika
barua
za watu wasiojua kuandika.
Kaligrafia
ni sanaa ya kuandika vizuri na kuremba maandishi. Hadi leo kuna waandishi wanaotekeleza kazi hii kama sanaa ama kwa kutunga kaligrafia za mapambo ya nyumba au kwa kutunga hati za pekee zinazotakwa kurembishwa.
Wengine wanajifunza kaligrafia kama
burudani
ya binafsi.
Katika
utamaduni
wa
Uyahudi
nakala za
Torati
kwa matumizi katika
ibada
ya
sinagogi
zinahitaji kuandikwa hadi leo kwa mkono: kuna waandishi walio mabingwa kwa shughuli hii.
Mnamo
1970
mwanamuziki
wa
jazz
Herbie Hancock
alianza kutumia jina "mwandishi" akaita
bendi
yake "Mwandishi" na kutoa
albamu
kwa jina hilo.
[4]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- ↑
Ake W. Sjoberg, In Praise of the Scribal Art, Journal of Cuneiform Studies 24/4, 1972, 26-131
- ↑
Brian E. Colless, Divine Education. Numen 17/2, 1970, 120f.
- ↑
David McLain Carr, Writing on the Tablet of the Heart: Origins of Scripture and Literature, Oxford University Press 2005,
ISBN 0-19-517297-3
, p.66
- ↑
https://nickdimaria.wordpress.com/2014/05/16/my-masters-thesis-on-herbie-hancocks-mwandishi-band/