Antonio Caetano de Abreu Freire Egas Moniz ( 29 Novemba 1874 ? 13 Desemba 1955 ) alikuwa daktari na mwanasiasa kutoka nchi ya Ureno . Hasa alichunguza neva za ubongo . Katika siasa alikuwa balozi ya Ureno kwa Hispania (miaka ya 1917 na 1918) na mwakilishi wa nchi yake kwenye mikutano ya kimataifa. Mwaka wa 1949 , pamoja na Walter Hess alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba .