Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia
Kiwanda (maana)
Kiwanda
ni mahali ambapo
bidhaa
mbalimbali hutengenezwa, yaani penye
majengo
na
mashine
. Bidhaa hizo zinaweza kuwa
ndoo
,
sahani
,
mabakuli
,
vijiko
,
masufuria
,
magari
,
kompyuta
,
bati
,
vyakula
mbalimbali,
nyundo
,
pasi
,
baiskeli
,
pikipiki
na
vitu
mbalimbali kwa ujumla. Hivyo kuna aina mbalimbali za viwanda: vipo viwanda vya vyakula, vya magari, vya
vifaa vya ujenzi
, vya
vyombo
mbalimbali, na vya vitu vizito, vya vyuma n.k.
Historia
Viwanda vilisambaa hasa kuanzia
karne ya 19
wakati wa
Mapinduzi ya viwandani
ambako
uzalishaji
wa bidhaa ulihamishwa kutoka
karakana
za
mafundi
kwenda
taasisi
kubwa zaidi ambako mashine pamoja na mpangilio wa
kazi
viliongeza tija ya uzalishaji.
Ugunduzi wa
injini ya mvuke
uliunda msingi wa matumizi ya mashine katika shughuli nyingi za uzalishaji. Pamoja na hayo, mashine hizi zilikuwa na
gharama
kubwa, hivyo ulimbikizaji wa
rasilmali
uliunda
tabaka
mpya ya
mabepari
.
Kuenea kwa viwanda kulisababisha mabadiliko makubwa katika
jamii
za
dunia
. Mafundi wa weledi nyingi walipoteza nafasi zao kwa sababu bidhaa zilitengenezwa sasa kwa
bei
nafuu na katika
muda
mfupi, mara nyingi pia kwa
ubora
mkubwa kuliko jinsi mafundi walivyoweza kuzitoa kwa
kazi ya mikono
. Lakini viwanda vimeleta pia kazi mpya na
ufundi
tofauti na awali.
Uzalishaji wa bidhaa katika viwanda umekuwa msingi muhimu wa mchakato wa
utandawazi
ambako bidhaa nyingi zinazalishwa katika nchi fulani na kuuzwa kote
duniani
ilhali vipuli vya kutengenezea bidhaa hizi tena zinatoka katika nchi tofauti.
Zipo nchi zenye viwanda vingi zaidi; nchi yenye viwanda vingi ni nchi tajiri, kwa mfano
Japani
. Viwanda vyake ni vya kutengeneza bidhaa kubwa na nzito zaidi, kama vile
meli
,
ndege
,
treni
, magari n.k.
Faida na hasara
Kila nchi ina viwanda mbalimbali. Viwanda hivyo huisaidia nchi hiyo pindi iuzapo bidhaa hizo, pia huisaidia nchi husika kunufaika kiuchumi kwa uwepo wa viwanda hivyo.
Viwanda vina
faida
kubwa sana katika nchi yenye viwanda hivyo; faida hizo ni:
- 1) Kuisaidia nchi kukua kiuchumi,
- 2) kupata
fedha za kigeni
,
- 3) kulipa
madeni
wanayodaiwa,
- 4) kuajiri watu ambao hawana
kazi
,
- 5) na kunufaisha
taifa
kwa ujumla n.k.
Tunapokuwa na viwanda tunanufaika kwa vitu vingi. Lakini viwanda vina madhara pia, tena mengi sana. Madhara hayo ni:
Kwa hiyo tuvitunze viwanda vyetu ili vilete faida, si kuangamiza watu na viumbe wengine.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
uchumi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kiwanda
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|