Robert William Holley ( 28 Januari 1922 ? 11 Februari 1993 ) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani . Hasa alichunguza usanisi wa protini ndani ya mwili wa binadamu. Mwaka wa 1968 , pamoja na Har Khorana na Marshall Nirenberg alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba .