Jina la kuzaliwa lilikuwa
Anna Hoss
, mtoto wa sita kati ya nane wa Matthias Hoss na Lucia Hoermann. Kati yao watatu tu walifikia
utu uzima
.
Anna alilelewa Kikristo sana, na tangu
utotoni
aliamua kuwa
mtawa
katika
monasteri
jirani ya
Meierhof
. Alikuwa akisali mara nyingi katika
kikanisa
chake, lakini
ufukara
wa
baba
yake haukumwezesha kutoa
mahari
iliyojitajika ili kukubaliwa.
Tofauti na monasteri za
Waklara
, zile za Utawa Hasa wa Tatu wa Mt. Fransisko zilikuwa chini ya
askofu
wa
jimbo
husika, na pengine zilikuwa na
utendaji
nje ya nyumba, kama vile kuhudumia
maskini
na
wagonjwa
. Lakini ile ya Kaufbeuren ililenga
sala
tu.
Mwaka
1703
Meya
wa Kaufbeuren, akiwa
Mprotestanti
, aliisaidia monasteri kwa kununua kilabu cha jirani kilichokuwa kinavuruga
utulivu
wa masista akawapa jengo kama zawadi kwa sharti la kumpokea Anna jumuiani.
[3]
Hivyo mnamo Juni mwaka huo Anna alipokewa, ila alitazamwa na wengi kama "mnyonyaji" kwa sababu ya kutoleta mahari. Paoja na hayo, Anna alipokea
kanzu
na
jina la kitawa
Maria Kresensya
.
Mwanzoni alidhulumiwa kwa namna mbalimbali, kama vile kutukanwa, kuagizwa
kazi
duni zaidi, na kunyang'anywa
chumba
. Hivyo ilimbidi kuomba wenzake wamruhusu kulala katika pembe la vyumba vyao.
Hatimaye Kresensya aliruhusiwa kuweka
nadhiri
na kuwa
mwanajumuia
kamili. Hasa alipangiwa kazi za
jikoni
.
Mwaka
1707
, alichaguliwa mkubwa mpya aliyempenda zaidi Kresensya, ambaye alipewa hivyo kazi muhimu ya
bawabu
, na mwaka
1717
ile ya
mlezi wa wanovisi
.
[3]
Wakati huo alikuwa ameshaanza kuwa
mwandishi
wa
barua
nyingi, zenye ma
shauri
kwa watu wa matabaka yote.
Ingawa
maradhi
yalizidi kumtesa, hata kupooza, mwaka
1741
alichaguliwa kuwa mkubwa wa nyumba,
wadhifa
aliokuwanao hadi
kifo
chake, tarehe 5 Aprili 1744.
[3]
[4]
Katika miaka hiyo michache ya
uongozi
, Kresensya aliinua hali ya kiroho ya monasteri kwa
imani
yake kubwa kwa
Maongozi ya Mungu
, utayari wa kuhudumia jumuia, utunzaji wa
kimya
, ibada kwa
Msulubiwa
Yesu na kwa
Ekaristi
tena kwa heshima kwa
Bikira Maria
.
Alihimiza masista kutumia
Injili
ili kulisha
maisha ya kiroho
, akichuja sana waliotaka kujiunga, kwa kusema: "
Mungu
anataka monasteri iwe
tajiri
kwa
maadili
, si kwa
mali
".
Alijitahidi hasa kuwashirikisha wengine
ari
yake kwa
heshima
ya
Roho Mtakatifu
.
Alipotangazwa mtakatifu, monasteri ilibadilishiwa jina na kuitwa kwa lile la Mt. Kresensya.
[5]