Karoli Borromeo alizaliwa katika mji wa
Arona
katika mkoa wa
Lombardia
nchini
Italia
mwaka
1538
.
Baada ya kupata
shahada
ya tatu katika
sheria
za
serikali
na za
Kanisa
, alifanywa
kardinali
na
mjomba
wake,
Papa Pius IV
, akachaguliwa kuwa
askofu mkuu
wa
Milano
.
Hata hivyo aliishi maisha magumu ya kifukara, hata alifananishwa kwa
mbwa
katika nyumba ya bwana wake.
Alikuwa
mchungaji
bora wa kundi lake. Mara kwa mara alipitia
parokia
zote
jimboni
mwake, aliitisha mikutano, hasa
sinodi
11, aliweka sheria za kufaa kwa watu, na alijitahidi kuhimiza
maadili
ya Kikristo.
Alitoa huduma nyingi kwa
maskini
, kama vile
shule
za bure,
mabweni
, nyumba za
wasichana
ili kuwatoa katika
ukahaba
, n.k.
Ndiye aliyefanikisha zaidi sehemu ya mwisho wa
Mtaguso wa Trento
na utekelezaji wake, kama vile uanzishaji wa
seminari
kwa ajili ya
malezi
ya
mapadri
wapya.
Alianzisha pia shirika la
Oratorio
jimboni mwake.
Alifariki dunia tarehe
3 Novemba
1584
.
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1562
- A. Sala,
Documenti circa la vita e la gesta di Borromeo
(4 vols., Milan: 1857?1859)
- Chanoine Silvain,
Histoire de St Charles Borromeo
(Milan: 1884)
- A. Cantono, "Un grande riformatore del secolo XVI" (Florence: 1904); "Borromus" in Herzog-Hauck,
Realencyklopadie
(Leipzig: 1897).
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- The Life of St. Charles Borromeo, Confessor and Archbishop of Milan
Archived
5 Machi 2016 at the
Wayback Machine
.
- University of San Carlos, Cebu City, Philippines Official Site
Archived
29 Novemba 2020 at the
Wayback Machine
.
- Saint Charles Borromeo Seminary
, Archdiocese of Philadelphia
- Pietro Canetta, "Biography of Carlo Borromeo" (in Italian)
,
Magazzeno Storico Verbanese
- "St. Charles Borromeo"
,
Catholic Encyclopedia
- "St. Charles Borromeo, Cardinal, Archbishop of Milan, Confessor"
,
Butler's Lives of the Saints
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|