Australia
ni
bara
pia ni
nchi huru
ya
Oceania
. Ikiwa na eneo la
km²
7,617,930 ni
bara
dogo kuliko yote
duniani
, na ni
kisiwa
kikubwa kuliko vyote. Kama nchi ni ya sita kwa ukubwa.
Commonwealth of Australia
Jumuiya ya Australia
|
Kaulimbiu ya taifa:
(hakuna)
|
Wimbo wa taifa
:
Advance Australia Fair
Wimbo la kifalme
:
God Save the Queen
|
|
Mji mkuu
|
Canberra
35°15′?S 149°28′?E
|
Mji?mkubwa?nchini
|
Sydney
|
Lugha?rasmi
|
Kiingereza
(
hali halisi, si kisheria
)
1
|
Serikali
|
Shirikisho
la
bunge
;
ufalme
wa kikatiba
1:
Charles III wa Uingereza
,
2:
Peter Cosgrove
,
3:
Scott Morrison
|
Uhuru
Katiba ya Australia
|
1.1. 1901
|
Eneo
?- Jumla
?- Maji (%)
|
7,617,930?km²
?(ya 6)
1
|
Idadi ya watu
?-
2022
kadirio
?-
2021
sensa
?- Msongamano wa watu
|
25,970,200 (53rd)
25,422,788
3.4/km² (192nd)
|
Fedha
|
Australian dollar
(
AUD
)
|
Saa za eneo
?- Kiangazi?(
DST
)
|
various
2
(
UTC
+8?+10)
various
2
(
UTC
+8?+11)
|
Intaneti TLD
|
.au
|
Kodi ya simu
|
+61
|
1
English does not have
de jure
official status (
source
)
2
There are some minor variations from these three time zones, see
Time in Australia
|
Iko
kusini
kwa
Indonesia
na
Papua Guinea Mpya
na iko
magharibi
kwa
New Zealand
. Mara nyingi visiwa vya New Zealand huhesabiwa kuwa sehemu ya bara la Australia. Vilevile Australia huangaliwa pamoja na visiwa vya
Pasifiki
katika orodha ya mabara ya dunia kama "
Australia na Pasifiki
".
Idadi
ya wakazi ni 25,970,200 (
mwaka
2022
).
Bara la Australia linakaa juu ya sehemu imara ya
bamba la Australia
bila mipaka ya
gandunia
na kwa hiyo hakuna
volkeno
;
matetemeko ya ardhi
ni madogo tu.
Umbali
kati ya magharibi na
mashariki
ni
km
4,000, na kati ya
kaskazini
na kusini umbali ni km 3,700.
Australia huzungukwa na
bahari ya Hindi
, bahari ya
Pasifiki
na
Bahari ya Kusini
. Kwa jumla ina
pwani
yenye
urefu
wa
kilomita
34,218.
Great Barrier Reef
mbele ya pwani ya mashariki-kaskazini ni vipwa vya
matumbawe
vikubwa duniani; ina urefu wa kilomita 2,000.
Sehemu kubwa ya bara ni
jangwa
au maeneo
yabisi
sana. Takriban
asilimia
40 ya eneo limefunikwa na
matuta ya mchanga
.
Ardhi
yenye
rutuba
iko kusini-mashariki na
kona
ya kusini-magharibi pamoja na
hali ya hewa
isiyo na
joto kali
. Hali ya hewa kaskazini ni ya
kitropiki
na huko kuna
misitu
minene pamoja na
savana
na jangwa.
Sehemu kubwa ya uso wa nchi ni
tambarare
na majangwa. Kwenye pwani ya mashariki na pia upande wa magharibi kuna
safu za milima
inayopanda hadi
kimo
cha
mita
2,200. Sehemu ya juu kabisa huitwa
milima ya theluji
au
Alpi za Australia
na
mlima Kosciuszko
unafikia kimo cha mita 2,229. Huko kuna
barafuto
za kudumu.
Sehemu ya chini iko kwenye
beseni
la
ziwa Eyre
iliyopo mita 17 chini ya
usawa wa bahari
. Tako la beseni hilo mara nyingi ni kavu kabisa, huwa pamejaa
maji
mara chache tu baada ya
mvua
kubwa sana.
Mahali pakavu kabisa ni
jangwa la Simpson
lenye
usimbishaji
chini ya 200
mm
kwa
mwaka
.
Mito
muhimu inaanza katika Alpi za Australia: ni
Murray
na
Darling
inayomwagilia
beseni
la Murray-Darling na hii ni eneo muhimu la
kilimo
cha Australia.
Mingine ni
Mto Snowy
na
Mto Murrumbidgee
, halafu
mto Fitzroy
(
Queensland
),
mto Ord
,
mto Swan
(
Australia ya Magharibi
),
mto Derwent
,
mto Tamar
(Tasmania) na
mto Hawkesbury
(
New South Wales
).
Sehemu kubwa ya bara haina watu. Wakazi wengi pamoja na miji yote wako kwenye pwani ya mashariki na kusini.
Miji
mikubwa ni
Sydney
(wakazi milioni 3.7),
Melbourne
(wakazi milioni 3.6),
Brisbane
(wakazi milioni 1.7),
Perth
(wakazi milioni 1.4) na
Adelaide
(wakazi milioni 1.1).
Mji mkuu
,
Canberra
(wakazi 308,700), ulijengwa kati ya Sydney na Melbourne kwa sababu miji hiyo miwili ilishindwa kukubaliana ni upi unaostahili kuwa mji mkuu.
Uchumi
katika maeneo yabisi ni hasa
ufugaji
wa
kondoo
milioni
130 na
ng'ombe
milioni 25.
Australia ilitengana na mabara mengine miaka milioni mingi iliyopita. Kwa sababu hiyo kuna aina nyingi za pekee za
mimea
na
wanyama
zisizopatikana penginepo duniani. Wanyama wa pekee ni kwa mfano
kanguru
na
koala
.
Miti
ya Australia kama vile
mkalitusi
imepelekwa kote duniani katika nchi zenye hali ya hewa ya kufaa.
Muundo
wa utawala ni wa
shirikisho
. Kuna ma
jimbo
6 ya kujitawala pamoja na maeneo ambayo yako moja kwa moja chini ya serikali ya shirikisho.
- Davison, Graeme; Hirst, John;
Macintyre, Stuart
(1999).
The Oxford Companion to Australian History
. Melbourne, Vic.: Oxford University Press.
ISBN
0-19-553597-9
.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
)
- Jupp, James (2001).
The Australian people: an encyclopedia of the nation, its people, and their origins
.
Cambridge University Press
.
ISBN
0-521-80789-1
.
- Smith, Bernard; Smith, Terry (1991).
Australian painting 1788?1990
. Melbourne, Vic.: Oxford University Press.
ISBN
0-19-554901-5
.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
)
- Teo, Hsu-Ming; White, Richard (2003).
Cultural history in Australia
.
University of New South Wales Press
.
ISBN
0-86840-589-2
.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
)
- Denoon, Donald, et al. (2000).
A History of Australia, New Zealand, and the Pacific
. Oxford: Blackwell.
ISBN 0-631-17962-3
- Goad, Philip and Julie Willis (eds) (2011).
The Encyclopedia of Australian Architecture
Cambridge University Press, Port Melbourne, Victoria.
ISBN 978-0-521-88857-8
- Hughes, Robert (1986).
The Fatal Shore: The Epic of Australia's Founding
. Knopf.
ISBN 0-394-50668-5
.
- Powell JM (1988).
An Historical Geography of Modern Australia: The Restive Fringe
. Cambridge, U.K.: Cambridge University Press.
ISBN 0-521-25619-4
- Robinson GM, Loughran RJ, and Tranter PJ (2000)
Australia and New Zealand: economy, society and environment
. London: Arnold; NY: OUP; 0340720336 paper 0-340720328 hard.
|
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
|
- ↑
Clarkson, Chris; Jacobs, Zenobia; Marwick, Ben; Fullagar, Richard; Wallis, Lynley; Smith, Mike; Roberts, Richard G.; Hayes, Elspeth; Lowe, Kelsey; Carah, Xavier; Florin, S. Anna; McNeil, Jessica; Cox, Delyth; Arnold, Lee J.; Hua, Quan; Huntley, Jillian; Brand, Helen E. A.; Manne, Tiina; Fairbairn, Andrew; Shulmeister, James; Lyle, Lindsey; Salinas, Makiah; Page, Mara; Connell, Kate; Park, Gayoung; Norman, Kasih; Murphy, Tessa; Pardoe, Colin (2017). "Human occupation of northern Australia by 65,000 years ago". Nature. 547 (7663): 306?310. Bibcode:2017Natur.547..306C. doi:10.1038/nature22968. hdl:2440/107043. ISSN 0028-0836.
PMID 28726833
.