Jean Nicolas Arthur Rimbaud
(
20 Oktoba
1854
-
10 Novemba
1891
) alikuwa mshairi kutoka nchini
Ufaransa
. Alizaliwa kama mtoto wa mwanjeshi huko Charleville katika kaskazini-mashariki ya Ufaransa. Wakati wa
vita ya Ujerumani dhidi ya Ufaransa ya 1870/71
alijitolea kuwa mwanajeshi akiwa na umri mdogo wa miaka 16 tu. Wakati uke aklianza kuandika mashairi yaliyohusu mwanzoni alichoona vitani.
Wakati ule alijitambua kuwa alivutiwa na jinsia ya kiume aka na uhusiano wa kipenzi na mshairi Paul Verlaine mkubwa wake.
Kati ya 1873 hadi 1873 alitoa vitabu 2 vya mashairi lakini alipofikia miaka 21 aliacha kuandika akaanza kuzunguka duniani. Alikaa miaka mingi
Afrika ya Kaskazini
na kwenye nchi kando la
Bahari ya Shamu
kama vile
Yemen
na
Uhabeshi
. Alifanya biashara ya
kahawa
,
dhahabu
,
meno ya tembo
na
silaha
. Kwa muda wa miaka saba alikaa mjini
Harar
alipokuwa rafiki wa gavana
Ras Makonnen
baba wa
Haile Selassie
aliyekuwa baadaye
Negus
wa Uhabeshi.
1891 aligonjeka goti akaona vema kurudi Ufaransa kwa tiba; mguu wake ulikatwa na madaktari lakini sababu ya ugonjwa ilikuwa kansa ya mfupa akafa tar. 10 Novemba 1891 mjini
Marseille
akiwa na umri wa miaka 37.