한국   대만   중국   일본 
Shirika la Mkombozi - Wikipedia, kamusi elezo huru

Shirika la Mkombozi

Shirika la Mkombozi Mtakatifu sana (kwa [[Kilatini: Congregatio Sanctissimi Redemptoris ? Ufupisho: C.Ss.R au CSSR) ni shirika la kitawa la kimisionari la Kanisa Katoliki lililoanzishwa na Alfonso Maria wa Liguori tarehe 9 Novemba 1732 huko Scala (karibu na Amalfi , Italia ) ili kushughulikia watu waliosahaulika wa mkoa wa Napoli .

Mt. Alfonso Maria wa Liguori (1696-1787), Mwanzilishi wa shirika
Mt. John Nepomucene Neumann (1811-1860), askofu wa kwanza wa Marekani kutangazwa mtakatifu

Kwa Kiingereza wanashirika wanajulikana kama Redemptorists . Wakiwa mapadri na mabradha wanafanya kazi katika nchi zaidi ya 77 duniani kote. Mkuu wao anaitwa Michael Brehl.

Wanashirika maarufu

hariri

Viungo vya nje

hariri